Serikali mpya ya Tunisia yakutana | Matukio ya Kisiasa | DW | 21.01.2011
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Serikali mpya ya Tunisia yakutana

Serikali mpya ya mpito nchini Tunisia jana imefanya mkutano wake wa kwanza wa baraza la mawaziri.

default

Rais wa mpito wa Tunisia, Fouad Mebazaa

Mkutano huo umefanyika huku maandamano mapya ya kutaka kuondolewa viongozi wa serikali iliyopita ya rais aliyeondolewa madarakani, Zine El Abidine Ben Ali, yakiendelea.

Kabinettssitzung Interimsregierung Tunesien

Rais wa Tunisia, Fouad Mebazaa, wa pili kulia akiongoza kikao cha kwanza cha mawaziri

Mawaziri hao wamekubaliana kutoa msamaha kwa wafungwa wote wa kisiasa na kuvihalalisha vyama vya siasa na makundi yaliyokuwa yamepigwa marufuku.

Wakati huo huo, polisi katika mji mkuu wa Tunis, wamefyatua risasi za onyo kuwatawanya mamia ya waandamanaji karibu na makao makuu ya kilichokuwa chama tawala.

Mmoja kati ya wapinzani wakuu wanaoongoza nchini humo, Taoufik Ben Brik, ametangaza kugombea katika uchaguzi wa rais ambao serikali ya mpito imesema utakuwa huru na wa haki.

 • Tarehe 21.01.2011
 • Mwandishi Kabogo Grace Patricia
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/100J5
 • Tarehe 21.01.2011
 • Mwandishi Kabogo Grace Patricia
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/100J5

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com