Serikali kuu yahitaji mkopo mkubwa zaidi | Magazetini | DW | 26.01.2009
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Magazetini

Serikali kuu yahitaji mkopo mkubwa zaidi

Wahariri waonya mzigo wa madeni usije ukaikaba serikali kuu

default

Waziri wa fedha Peer Steinbrück
Wahariri wa magazeti ya Ujerumani wamejishughulisha zaidi hii leo na mzigo mpya wa madeni wa serikali kuu kwa mwaka huu wa 2009,mkutano mkuu wa chama cha walinzi wa mazingira "Die Grüne" na kubatilishwa na kiongozi wa kanisa katoliki ulimwenguni,Benedikt wa 16 amri ya kutengwa maaskofu wanne wanaofuata muongozo asilia.


Tuanze lakini na mzigo wa madeni unaoikabili serikali kuu kwa mwaka huu wa 2009.Serikali kuu ya Ujerumani inaelekea kujitwika mzigo mkubwa kabisa wa madeni kuwahi kushuhudiwa katika historia yake linaandika Gazeti la Die WELT na kuendelea:"Zaidi ya yuro bilioni 50 anabidi akope waziri wa fedha Peer Steinbrück.Kama si mzigo huo serikali inayojibebesha,basi ni nini?Jinamizi la kale linaanza kuchomoza na kukumbusha miaka ya 20 pale ughali wa maisha ulipokithiri.Uaminifu wa kupatiwa mikopo unapopotea ndipo nayo serikali inayodaiwa kope si zake inapokabiliwa na kitisho cha kufilisika.Hali kama hiyo imeonekana miaka michache nyuma nchini Argentina.Ujerumani lakini iko mbali na kuifikia hali kama hiyo kutisha.Mipango ya kuupiga jeki uchumi iliyotiwa njiani miaka ya nyuma imeanza kuleta tija.Ndio maana kuna umuhimu mkubwa wa kuzingatia malipo ya riba mkopo utakapochukuliwa katika wakati huu wa mzozo wa fedha.Gazeti la SÜDDEUTSCHE ZEITUNG linasema "kuna wakati hakuna njia isipokua kuzidishia madeni"-Gazeti linaendelea kuandika:


"Serikali inalazimika kutoa fedha nyingi zaidi kugharimia mpango wa kuinua shughuli za kiuchumi na kuunusuru mfumo wa kiuchumi usiporomoke.Watu wasizowee tuu.Mizigo mizito mizito ya madeni iruhusiwe tuu panapotokea  dharura.La sivyo uaminifu wa Ujerumani katika kupatiwa mikopo utaingia dowa.Ndio maana ni jambo la maana kumuona Steinbrück akiwakumbusha mawaziri wenzake juu ya umuhimu wa kutotumia fedha ovyo ovyo.


Kuhusu mkutano mkuu wa chama cha walinzi wa mazingira Die Grüne mjini Dortmund linaandika gazeti la LEIPZIGER VOLKSZEITUNG


"Asili mia 13.7 ya kura wamejikingia walinzi wa mazingira katika uchaguzi wa Hesse.Ni matokeo ya kutia moyo hayo.Furaha yao imehanikiza pia katika mkutano wao mkuu wa mjini Dortmund ambako hawajakubali walinzi wa mazingira kuachana na mada kuhusu usafi wa hali ya hewa na uchumi unaoheshimu mazingira,kwa hoja za kudorora uchumi.Wamepania kuzuwia serikali ya vyama vya nyeusi na njano isiingie madarakani mjini Berlin.Wanataka pia kuleta mageuzi ya kisiasa katika bunge la Ulaya kwa kujikingia zaidi ya viti 13 katika bunge la mjini Brussels.


Gazeti la FRANKFURTER ALLGEMEINE linajishughulisha na kisa cha kubatilishwa amri ya   kutengwa maaskofu wanne wanaofuata nadharia asilia.Gazeti linaandika:


"Kwamba maaskofu hao wa "udugu wa Pius wamerejershewa vyeo na hadhi yao si jambo lililozuka vivi hivi tuu.Kiongozi wa kanisa katoliki ulimwenguni Benedikt was 16 ametekeleza nia ya kuleta suluhu pamoja na wafuasi wa askofu mkuu Lefebre wa Ufaransa.Nia hiyo amekua akiitetea tangu alipochaguliwa kuongoza kanisa katoliki ulimwenguni.


 • Tarehe 26.01.2009
 • Mwandishi Oumilkher Hamidou
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/GgK5
 • Tarehe 26.01.2009
 • Mwandishi Oumilkher Hamidou
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/GgK5
Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com