1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Serikali kuchunguza mauaji Afrika kusini

18 Agosti 2012

Rais wa Afrika kusini Jacob Zuma ametangaza Ijumaa (17.08.2012) kuunda kamati itakayochunguza vifo vya wachimba migodi 34 wakati polisi walipokuwa wakijaribu kuzima mgomo wa wafanyakazi hao wa migodi.

https://p.dw.com/p/15sBq
Striking miners chant slogans outside a South African mine in Rustenburg, 100 km (62 miles) northwest of Johannesburg, August 15, 2012. Thousands of striking miners armed with machetes and sticks faced off with South African police on Wednesday at Lonmin's Marikana mine after it halted production following the deaths of 10 people in fighting between rival unions. Lonmin, the world's third-largest platinum producer, has threatened to sack 3,000 rock drill operators if they fail to end a wildcat pay strike that started on Friday at its flagship mine Marikana. REUTERS/Siphiwe Sibeko (SOUTH AFRICA - Tags: CIVIL UNREST BUSINESS EMPLOYMENT TPX IMAGES OF THE DAY)
Wafanyakazi waliogoma wa mgodi wa MarikanaPicha: Reuters

Polisi katika mgodi wa madini ya Platinum wa Marikana unaoendeshwa na kampuni ya Lonmin , ambayo ni kampuni ya tatu duniani kuzalisha madini hayo, badala yake walichukua tahadhari ya kujilinda dhidi ya mamia ya wafanyakazi ambao walivamia huku wakishambuliwa kwa mabomu ya kutoa machozi na risasi za mpira wakijaribu kuwashambulia maafisa wa polisi kwa bunduki, mapanga na marungu.

Lakini taifa hilo lilijikunyata katika kile ambacho vyombo vya habari vimelieleza haraka tukio hilo kuwa ni "Mauaji ya Marikana", wakilinganisha tukio hilo na mauaji ya wakati wa enzi za utawala wa kibaguzi, hususan mauaji ya Sharpeville ya mwaka 1960 wakati polisi wa utawala huo wa wazungu walipowauwa waandamanaji 69.

Zuma asitisha ziara

Wakati idadi ya waliouwawa ikiongezeka jana , Zuma alifupisha ziara yake katika mkutano wa kimkoa na kurejea nyumbani na moja kwa moja alikwenda katika mgodi huo, akiaahidi kufichua sababu za mauaji hayo.

South African President Jacob Zuma attends 32nd summit of the Southern African Development Community (SADC) at Maputo's Joaquim Chissano Conference Centre on August 17, 2012 in Maputo. Southern African leaders meet until August 18 in Maputo for a summit that will try to nudge Madagascar and Zimbabwe toward new elections under 'roadmaps' that are a test of the region's commitment to democracy. Zuma will cut short his visit to Mozambique to visit the Lonmin Marikana mine in Rustenburg where up to 36 striking miners were killed in a clash with police yesterday. AFP PHOTO / STEPHANE DE SAKUTIN (Photo credit should read STEPHANE DE SAKUTIN/AFP/GettyImages)
Rais wa Afrika kusini Jacob ZumaPicha: AFP/Getty Images

Ni wazi kuwa kuna kitu nyuma ya matukio haya na ndio sababu nimechukua uamuzi huu wa kuunda tume ya uchunguzi, kwa sababu ni lazima tujue ukweli, Zuma amesema.

Hiki ni kitu kinachositua. Hatufahamu kinatokea wapi na ni lazima tufahamu. Hali hii haikubaliki nchini mwetu, ambayo ni nchi ambayo kila mtu anajisikia salama. Nchi ambayo ina demokrasia ambayo kila mtu anaionea kijicho.

Policemen react after firing shots at protesting miners outside a South African mine in Rustenburg, 100 km (62 miles) northwest of Johannesburg, August 16, 2012. South African police opened fire on Thursday against thousands of striking miners armed with machetes and sticks at Lonmin's Marikana platinum mine, leaving several bloodied corpses lying on the ground. A Reuters cameraman said he saw at least seven bodies after the shooting, which occurred when police laying out barricades of barbed wire were outflanked by some of an estimated 3,000 miners massed on a rocky outcrop near the mine, 100 km (60 miles) northwest of Johannesburg. REUTERS/Siphiwe Sibeko (SOUTH AFRICA - Tags: CIVIL UNREST CRIME LAW BUSINESS EMPLOYMENT)
Polisi wa Afrika kusini karibu na mgodi MarikanaPicha: Reuters

Marekani yasikitika

Ikulu ya Marekani , White House, imesema jana Ijumaa kuwa Marekani imesikitishwa na vifo na kueleza matumaini kuhusu uchunguzi wa serikali. Watu wa Marekani wamesikitishewa na vifo vilivyotokea , amesema naibu afisa wa habari wa ikulu ya Marekani Josh Earnest alipokuwa akizungumza na waandishi habari.

Women protest against the police near the scene of the shooting of miners Thursday at the Lonmin mine near Rustenburg, South Africa, Friday, Aug. 17, 2012. Frantic wives searched for missing loved ones, President Jacob Zuma rushed home from a regional summit and some miners vowed a fight to the death Friday as police finally announced the toll from the previous day’s shooting by officers of striking miners: 34 dead and 78 wounded. (Foto:Themba Hadebe/AP/dapd).
Ndugu wa wafanyakazi wa mgodi wa Marikana wakilalamika kwa polisiPicha: dapd

Tunaimani kuwa serikali ya Afrika kusini itachunguza mambo yaliyosababisha hali hii na kila wakati, tunazipa moyo pande zote kufanyakazi kwa pamoja kuipatia ufumbuzi hali hii kwa amani.

Mkuu wa polisi anena

Mkuu wa polisi Riah Phiyega amewakingia kifua maafisa wake wa polisi , akisema kuwa walitumia risasi baada ya majadiliano na mbinu za kulidhibiti kundi hilo la wachimba migodi kushindwa.

Kundi hilo la wanaharakati lilikimbia kuelekea kwa polisi, wakifyatua risasi na kuwa na silaha hatari, amesema. Polisi walirudi nyuma kimpango na walilazimika kutumia nguvu kiasi kujilinda. Hadi sasa watu 259 wamekamatwa kuhusiana na mapambano hayo ambayo yamesababisha watu 34 kuuwawa na wengine 78 wamejeruhiwa, amesema Phiyega.

Baadhi ya wafanyakazi wa mgodi huo walikuwa katika mgomo wa wiki moja wakidai nyongeza mara tatu ya mishahara yao kutoka randi 4,000 ambayo ni sawa na euro 400 kwa mwezi.

Mwandishi: Sekione Kitojo / afpe

Mhariri: Bruce Amani