1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Sera ya wakimbizi yawa mwiba nchini Ujerumani

Zainab Aziz
10 Februari 2017

Katika mwaka 2017 mpango wenye vipengele 16 wa Kansela Angela Merkel anataka kuibadili sera ya wakimbizi ya nchini Ujerumani kwa imani kwamba utakidhoofidha chama Mbadala kwa Ujerumani AfD.

https://p.dw.com/p/2XKD9
Merkel Gauck Appoints New Foreign Minister, Shifts In Other Cabinet Posts
Picha: Getty Images/S. Gallup

Tumtamkumbuke Kansela wa  zamani wa Ujerumani Helmut Kohl na mpango wake uliokuwa na vipengele kumi juu ya kuungana kwa pande mbili za Ujerumani. Hayo yalitokea mnamo mwezi  Novemba mwaka 1989,
Lakini kansela Merkel mwenyewe hawezi kufanya hivyo peke yake, hivyo basi ni  lazima majimbo yote hapa nchini yaingie pamoja naye katika jahazi lake kabla ya safari kuanza. Kwa kawaida lisingekuwa ni jambo rahisi kwa sababu serikali ya shirikisho na serikali za majimbo mara nyingi huwa  hazilingani  kwa sababu majimbo yanaongozwa na siasa za vyama tofauti na hivyo basi mitazamo ya kisiasa pia tofauti. Lakini mwaka huu wa 2017 kuna sababu muhimu kwa kuwepo na umoja.  Katika miezi ya Machi na Mei kutafanyika uchaguzi kwenye majimbo ya Saarland, Schleswig-Holstein na katika  jimbo la Kaskazini la Westfalia. Mwezi Septemba uchaguzi mkuu - Bundestag - utafanyika. Kama mambo yalivyo, chama mbadala kwa ajili ya Ujerumani cha mrengo wa kulia  AfD kina nafasi nzuri ya kuingia katika mabunge yote manne.
Sera ya wakimbizi na matokeo yake inazidi kutoa nafasi ya mafanikio ya kuchaguliwa kwa chama cha AfD. Si ajabu basi kuviona vyama vya  CDU/CSU, SPD na Kijani, vinavyotawala katika majimbo hayo matatu na katika serikali kuu ya shirikisho,vinajitahidi kuzuia mianya yote ili chama cha AfD kisipate upenyo. Kwa kutilia maanani kile kilichotokea mwaka na nusu uliopita ingawa haitakuwa kazi rahisi. Mengi yamejilimbikiza, mengi yameharibika na mengi yalipuuzwa.
Mwishoni mwa mwaka 2016 wahamiaji zaidi ya 207,000  walitakiwa kuondoka. Idadi hiyo inaweza pia  kuongezeka na kufikia hadi karibu nusu milioni ifikapo mwishoni mwa mwaka huu. Takwimu hizo zilitolewa na  washauri  wa kampuni ya McKinsey kwa niaba ya idara ya Shirikisho ya Uhamiaji na Wakimbizi (BAMF).  Hakika ni watu 85,000 tu wangeweza kufukuzwa nchini kila mwaka. Inakadiriwa kuwa kiasi cha Euro Bilioni tatu zingetumika kwa ajili ya watu waliokataliwa hifadhi ya kubakia nchini Ujerumani.   
Hali hii inasababisha kuwepo mlipuko wa kisiasa. Hasa baada ya mashambulizi ya kigaidi kwenye soko  Krismasi la mjini Berlin, yaliyofanywa na muhamiaji wa Kitunisia aliyepaswa kuondoka nchini Anis Amri. Mashambulizi  hayo kwa kiwango kikubwa yametumbua  hisia mbaya kwamba serikali  haina uwezo wa kushughulikia madhara yanayosababishwa na mgogoro wa wakimbizi.  Serikali imnaonekana kuwa imepoteza muelekeo na inashindwa kuhakikisha usalama, utii wa sheria na utaratibu kwa jumla na kwamba inatumiwa vibaya na wahalifu ambao wanasingizia kuwa ni wakimbizi. Kwa upande mwingine serikali haina nguvu.  Yote hayo ni kama mteremko kwa chama  kinachojiita cha mbadala kwa Ujerumani cha mrengo wa kulia  AfD.
watendaji katika serikali ya Shirikisho na katika majimbo wanatambua hatari zilizopo katika uchaguzi ujao. Hawakuchukua hata ta saa tatu katika mkutanobaina ya kansela Angela Merkel na mawaziri wakuu wa majimbo  katika ofisi ya kansela.  Kwa kiasi kikubwa walifikia makubaliano. "Hakuna Utani", hiyo ndio kauli mbiu waliofikia. Wanataka kuonyesha mshikamano wao, kuendelea mbele kwa pamoja bila kipingamizi chochote. "Siasa" kama inavyosemekana siku zote ni sawa na kuchimba polepole kwenye gogo nene. Lakini safari hii Inaonekana kifaa chenye nguvu zaidi kimetumika huko mjini Berlin.
Jinsi  shinikizo lilivyo kubwa serikali ya shirikisho inapaswa kwa siku za usoni kuandaa mapema stakabadhi za watu, kuratibu na pia kuwaweka kizuizini wahamiaji ambao wamenyimwa vibali vya kuishi. Pia inapaswa kutambua watu ambao ni tishio kwa usalama wa ndani wa hapa nchini Ujerumani lakini mpaka sasa jukumu hilo ni la majimbo tu. 
Wananchi, hata hivyo, hawajali nani hasa anawajibika kufanya nini  mwisho wa kuishia wanataka kuona wanasiasa wametekeleza nini katika sera walizozinadi. Wananchi wengi nchini Ujerumani wamechoshwa. Wengi mno kati ya Wajerumani wazawa na wageni walioishi nchini humu kwa muda mrefu wanasema wanataka suluhisho lipatikane.   Hofu ya uhalifu na kupatikana kwa mahitaji muhimu ndio inazidi kuongezeka miongoni mwa Waajerumani.

Hannover  AfD-Landesparteitag Wilhelm von Gottberg Alexander Gauland
Viongozi wa chama mbadala kwa Ujerumani AfDPicha: picture-alliance/dpa/P. von Ditfurth

Mwandishi Zainab Aziz/ Kinkartz, Sabine (HSB) LINK: http://www.dw.com/a-37487846
Mhariri:Josephat Charo