Sera ya Trump Mashariki ya Kati yadidimiza heshima ya Marekani | Matukio ya Kisiasa | DW | 18.01.2018
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Kisiasa

Sera ya Trump Mashariki ya Kati yadidimiza heshima ya Marekani

Kwa mwaka mmoja sasa Donald Trump ndie rais wa Marekani. Kwa ujumla sera yake ya Mashariki ya Kati inafuta ile ya watangulizi wake. Lakini baadhi ya maamuzi yake yameiporomosha heshima ya Marekani katika kanda hiyo.

Mwanzoni  mwa  mwezi  Desemba  mwaka jana  makamu  wa  rais  wa Marekani  Mike  Pence  alifuta  ziara  yake  katika  eneo  la  mashariki ya  kati. Sasa  amepanga  tena kuifanya  ziara  hiyo.

Wakati  ule  hali  ilikuwa  mbaya  sana, baada  ya   rais  wake Donald Trump  kuutambua  mji  wa  Jerusalem  kama  mji  mkuu  wa  Israel, na kutangaza azma ya kuuhamishia ubalozi  wa  Marekani  kutoka  Tel Aviv kwenda  Jerusalem.

Baada  ya  tangazo  hilo  heshima  ya  Marekani  katika  eneo  kubwa la   mataifa  ya  Kiarabu  iliporomoka. Hususan kwa  Wapalestina ambao  walijihisi  kwamba  maslahi  yao  hayakuangaliwa. Kwa  hiyo ilionekana  mjini  Washington  kama  ilivyo  katika miji  mikuu  ya mataifa ya  mashariki  ya  kati  kuwa  ni  busara  kwanza  kuiahirisha  ziara  hiyo hadi  wakati  mwingine  baadaye.

Ziara yaangukia mwaka mmoja wa Trump

Kwa  hivi  sasa   hali imetulia  na  tarehe  19. Januari  Pence anaanza ziara   hiyo.  Anatarajiwa  kufika   mjini  Jerusalem, Cairo  na  kama ilivyokubaliwa  atafika  pia  katika  mji  mkuu  wa  Jordan Amman.

Ziara  hiyo  ya  makamu  wa  rais  inaangukia  katika  siku  ambayo kunaadhimishwa  mwaka  mmoja  tangu  utawala  wa  Trump  kuingia madarakani, tarehe  20 Januari 2017.

Putin und Assad (Getty Images/AFP/M. Klimentyev)

Rais wa Syria Bashar al-Assad akisalimiana na rais wa Urusi, Vlamdir Putin walipokutana mwishoni mwa mwaka 2017.

Kimsingi  anasema  mtaalamu  wa  masuala  ya  mashariki  ya  kati Andre Bank  kutoka  katika  taasisi ya  utafiti  wa  masuala  ya mashariki  ya  kati  ya  GIGA  mjini  Hamburg, kwamba Trump ana mwelekeo  wake  katika  sera  za  mashariki  ya  kati, lakini  sio  kama watangulizi  wake.

"Sioni tofauti kubwa  katika  nyanja zingine isipokuwa katika  sera  za mambo  ya  kigeni, ukilinganisha  na  maeneo mengine. Kwa kulinganisha  na  rais  Obama  kwa  mfano  katika  sera  kuelekea mashariki  ya mbali , kumekuwa  na  mivutano  zaidi, hususan China. Kwa  upande  wa  Ulaya  hali imekuwa  mbaya  zaidi  tangu  Trump kuingia  madarakani.

Sera kuelekea Syria

Lakini kitu  cha  ajabu  ni  kwamba  katika  mashariki  ya  kati  na hususan  kuhusu  Syria  hakuna mengi  aliyobadilisha, ukilinganisha na utawala  wa  Obama. Na  inaonekana  Marekani  tayari inachukua sera ya  kujiweka  kando," anasema Bank.

Kuhusu Syria  mtangulizi  wa  Trump, rais Barack Obama  katika  kipindi chake  chote  cha  utawala alifuata  njia  ya  kujizuwia. Katikati  ya mwaka  2012  Obama  alitoa  onyo  kali  kwa  serikali  ya  Syria.

Wakitumia  gesi  ya  sumu  dhidi  ya  mahasimu  wake, itakuwa ni kuvuka  'mstari  mwekundu'. Rais  wa  Syria  Bashar al-Assad alionekana  hakustushwa  na  kauli  hiyo.

Hata  baada  ya  kutokea mashambulizi  ya  gesi  ya  sumu  Obama hakuchukua  hatua, na  badala  yake  aliwapa  tu waasi  silaha. Hata utawala  wa  Trump  nao  haukufanya  chochote  isipokuwa  kufuata mfano  wa  Obama, kwa  kupambana  na  kundi  linalojiita  Dola  la Kiislamu.

Ägypten palästinensischer President Mahmoud Abbas in Al-Azhars Konferenz zu Jerusalem (Reuters/M. Abd El Ghany)

Rais wa mamlaka ya Wapalestina Mahmoud Abbas akizungumza wakati wa chuo kikuu cha Azhar kuhusu Jerusalem, mjini Cairo, Misri, Januari 17,01.2018. Abbas alimshabulia Trump kwa uamuzi wake kuhusu Jerusalem.

Saudia yaafiki sera ya Trump

Waziri  wa  ulinzi  wa  Saudi Arabia  na  mwanamfalme  Mohammed bin Salman kwa  kuonesha  wazi  kuwapo  karibu  na  Trump  ameidhinisha sera zake.

Viongozi  hao  wawili  wanaonesha  kuaminiana, kwasababu  ya  wote wanamtazamo  hasimu  na  Iran, ikiwa  ni  nchi  yenye ushindani mkubwa nana Saudi Arabia kuwania ushawishi katika  eneo  la Mashariki ya Kati.

Rais wa Marekani, anasema  mtaalamu  wa  masuala  ya  Saudi Arabia Sebastian Sons  kutoka  taasisi  ya  Ujerumani  inayojishughulisha  na masuala  ya  kigeni , na viongozi  hao  wana msimamo  mmoja  kuhusu mzozo  wa  Jemen.

Mwandishi : Knipp, Kersten / Sekione  Kitojo

Mhariri: Gakuba, Daniel

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com