1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

SEOUL: Ujumbe wa Marekani wawasili Korea Kusini

10 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBRA

Ujumbe wa serikali ya Marekani unatarajiwa kuwasili Korea Kusini hii leo kabla kufanya ziara rasmi nchini Korea Kaskazini kuchunguza vinu vya nyuklia vinavyotakiwa kufungwa.

Ujumbe wa Marekani unaongozwa na Sung Kim, afisa wa wizara ya mambo ya ndani ya Marekani, anayeshughulikia maswala ya Korea.

Ujumbe huo utakutana na maafisa wa Korea Kusini hii leo mjini Seoul kabla kusafiri kwenda Korea Kaskazini kupitia kijiji cha mpakani cha Panmunjon. Ziara ya siku tano nchini Korea Kaskazini itakayoanza kesho Jumanne, ni hatua ya kwanza kufuatilia makubaliano ya hivi karibuni kati ya Marekani na Korea Kaskazini yaliyofikiwa kwenye mkutano wa mjini Geneva, Uswisi.

Katika mkutano huo Korea Kaskazini iliahidi kuwa wazi na kuvifunga vinu vyake vya nyuklia kufikia mwishoni mwa mwaka huu.

Korea Kaskazini iliwaalika wataaalmu wa nyuklia kutoka Marekani, China na Urusi kwenye mkutano wa mjini Geneva mwanzoni mwa mwezi huu. Wizara ya mambo ya kigeni ya Korea Kusini imekataa kuthibitisha taarifa hizo.

Msemaji wa ubalozi wa Marekani mjini Seoul pia amekataa kusema lolote kuhusu ziara ya ujumbe huo wa Marekani.