SEOUL: Madai ya Korea Kaskazini yametiliwa chumvi | Habari za Ulimwengu | DW | 11.10.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

SEOUL: Madai ya Korea Kaskazini yametiliwa chumvi

Rais wa Korea Kusini, Roh Moo-Hyun, leo amesema madai ya Korea Kaskazini kwamba inakabiliwa na hatari ya kuvamiwa aidha yametiliwa chumvi au hayana msingi wowote.

Matamshi hayo ni ya kwanza ya Korea Kusini kuupinga utawala wa kikomunisti wa Korea Kaskazini na yametofautiana na matamshi ya rais Roh ya mwaka wa 2004 aliposema madai ya Korea Kaskazini kwamba mpango wake wa nyuklia ulikuwa sehemu ya juhudi za kujilinda dhidi ya vitisho kutoka nje, yalikuwa na ukweli.

Akihutubia mkutano wa washauri wa sera ya muungano mjini Seoul hii leo, rais Roh Moo-Hyun amesema ikiwa Korea Kaskazini inataka amani na usalama wa kweli, kutengeza silaha ni muhimu lakini sharti idumishe amani na kuaminiana na mataifa jirani.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com