1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Senegal yatwaa tena kombe la AFCON

19 Januari 2026

Senegal imeshinda Kombe la Mataifa ya Afrika, AFCON, katika kile kinachotajwa kuwa fainali ya vituko.

https://p.dw.com/p/571wP
AFCON 2025 | Fainali | Senegal vs. Moroko | Sadio Mané
Nahodha wa timu ya taifa ya Senegal, Sadio Mane, akinyanyuwa kombe baada ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Moroko kwenye michuano ya fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika mjini Rabat siku ya Jumapili (Januari 18, 2026).Picha: Siphiwe Sibeko/REUTERS

Pape Gueye aliwapatia Teranga Boys bao pekee la ushindi kwenye muda wa nyongeza kwenye mechi hiyo ambayo ilishuhudia wachezaji wa Senegal kutishia kutoka uwanjani na mashabiki wake kuvamia uwanja wakilalamikia adhabu ya mkwaju wa penalti kwenye kipindi cha pili cha mchezo huo.

Ilichukuwa takribani robo saa kwa wachezaji wa Senegal kurudi uwanjani, ambapo kipa wa Senegal, Édouard Mendy aliunyaka mkwaju wa Brahim Díaz wa Moroko kirahisi.

Gueye alitia kimiani goli la ushindi kwenye dakika ya nne katika muda wa ziada.

Uwanja wa Mwanamfalme Moulay Abdellah wenye uwezo wa kuchukuwa mashabiki 69,500 ulikuwa takribani mtupu muda mchache tu baada ya fainali hizo kumalizika, na wachache ndio waliosalia kuwashuhudia Wasenegali wakibeba kombe lao.

Hii ni mara ya pili kwa Teranga Boys kutwaa kombe hilo, mara ya mwisho ikiwa ni mwaka 2021 walipoiangusha Misri kwa matuta.