1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Senegal yapigwa faini na FIFA

Bruce Amani
2 Mei 2022

FIFA yaipiga shirikisho la kandanda la Senegal faini ya faranga za Kiswisi 175,000 sawa na dola 180,000 kwa utovu wa nidhamu wa mashabiki katika mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia

https://p.dw.com/p/4AjpN
WM Qualifikation Ägypten Senegal
Picha: Ahmed Gomaa/Xinhua News Agency/picture alliance

FIFA yaipiga shirikisho la kandanda la Senegal faini ya faranga za Kiswisi 175,000 sawa na dola 180,000 kwa utovu wa nidhamu wa mashabiki katika mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia, ikiwemo kummulika usoni miale nyota wa Misri Mohamed Salah wakati wa kupigwa matuta.

Uso wa Salah ulimulikwa na miale ya kijani wakati akijiandaa kupiga mkwaju wa penati, ambao kisha ulipaa juu ya besela. Senegal walishinda kwa penalty mjini Dakar mwezi Machi huku mchezaji mwenza wa Salah katika klabu ya Liverpool Sadio Mane akifunga penalti ya ushindi.

FIFA imesema kamati yake ya nidhamu pia imezingatia uvamizi uliofanywa na mashabiki wa Senegal uwanjani, bango lililokuwa na ujumbe wa kukera, na kushindwa kwa shirikisho la kandanda kushindwa kuhakikisha amani na utulivu inadumu uwanjani. Senegal pia imeamuriwa kucheza mechi moja ya ushindani katika siku za usoni bila mashabiki.

afp