1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Senegal yakwanza kufuzu fainali za AFCON 2022

Sylvia Mwehozi
16 Novemba 2020

Senegal imekuwa timu ya kwanza kufuzu michuano ya kombe la mataifa ya Afrika Afcon kwa mwaka 2022 baada ya mshambuliaji wake Sadio Mane kuipatia timu hiyo bao 1 la ushindi dhidi ya Guinea-Bissau

https://p.dw.com/p/3lM1l
Sadio Mané I Trikot Senegal
Picha: Celso Bayo/ZUMA/picture alliance

Senegal imekuwa timu ya kwanza kufuzu michuano ya kombe la mataifa ya Afrika Afcon kwa mwaka 2022 baada ya mshambuliaji wake Sadio Mane kuipatia timu hiyo bao 1 la ushindi dhidi ya Guinea-Bissau katika mechi iliyochezwa jana Jumapili.

Senegal ilipoteza dhidi ya Algeria katika fainali za michuano hiyo iliyofanyika nchini Misri mwaka uliopita.

Bingwa mtetezi Algeria, Ghana na Tunisia zote zimeshinda michezo mitatu na zinaweza kuungana na Senegal katika kufuzu fainali za michuano hiyo ya kandanda barani Afrika.

Hivi leo Algeria itachuana na Zimbabwe, wakati Ghana itakabana koo na Sudan na Tunisia ina miadi naTanzania katika mchezo utakaopigwa kesho Jumanne.

Katika makundi mengine, Comoro imeendeleza ndoto ya kutaka kufuzu michuano hiyo baada ya kuichapa Kenya 2-1 na kuongoza kundi G.

Fainali za michuano hiyo zilikuwa zifanyike hapo mwakani lakini zimesogezwa hadi 2022 kutokana na janga la virusi vya corona.