Sebastian Vettel akaribia taji la ubingwa wa dunia | Michezo | DW | 23.09.2013
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Sebastian Vettel akaribia taji la ubingwa wa dunia

Sebastian Vettel anapuuza vitendo vinavyoendelea kushuhudiwa vya kusomewa na mashabiki baada ya ushindi wake wa mfululizo, na badala yake kuviona kama pongezi kutoka kwa mashabiki wenye wivu wa timu ya Ferrari.

SINGAPORE - SEPTEMBER 22: Sebastian Vettel of Germany and Infiniti Red Bull racing lifts the trophy following his victory during the Singapore Formula One Grand Prix at Marina Bay Street Circuit on September 22, 2013 in Singapore, Singapore. (Photo by Mark Thompson/Getty Images)

Formel 1 Großer Preis von singapur

Dereva huyo wa timu ya Red Bull alizomewa tena na mashabiki wa Formula One, wakati akifanyiwa mahojiano jukwaani baada ya kuwapiku wapinzani wake kwa mara nyingine katika mkondo wa Singapore Grand Prix jana Jumapili.

Kutawala kwa Vettel ambako nyota wa timu ya Ferrari, Fernando Alonso anaendelea kukifuata kivuli chake akiwa katika nafasi ya pili, na pia tukio lenye utata ambalo Vettel alipuuza maagizo ya wasimamizi wake na kumpiku dereva mwenzake wa RED Bull Mark Webber mapema msimu huu katika mkondo wa Malaysia huenda ndizo sababu zinazowanya mashabiki kumzomea Mjerumani huyo.

Viongozi wa Red Bull wanakashifu hatua hiyo, ijapokuwa Vettel anasema hajalishwi na matukio hayo…Vettel sasa anaongoza msimamo wa madereva, akiwa na mwanya wa pointi 60 mbele ya nambari mbili Alonso, huku kukisalia mikondo sita msimu kukamilika.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/Reuters

Mhariri: Yusuf Saumu