Schweinsteiger mwanasoka bora wa Ujerumani 2010 | Michezo | DW | 29.12.2010
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Schweinsteiger mwanasoka bora wa Ujerumani 2010

Jogoo wa mabingwa wa Ujerumani Bayern Munich Bastian Schweinsteiger amechaguliwa kuwa mwanasoka bora wa mwaka nchini Ujerumani

Bastian Schweinsteiger

Bastian Schweinsteiger

Schweinsteiger, kiungo imara, alichaguliwa na jarida maarufu la michezo nchini Ujerumani, Kicker, kuwa mwanasoka bora kabisa katika mwaka 2010.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 alikuwa miongoni mwa wachezaji waliochomoza na kuonesha kandanda la hali juu katika fainali za kombe la dunia mwaka huu nchini Afrika Kusini, ambapo Ujerumani ilifikia nusufainali.

Amecheza mechi 223 katika ligi ya Ujerumani, Bundesliga, na ameshinda ubingwa wa ligi hiyo mara tano pamoja na kombe la shirikisho la soka la Ujerumani tokea alipojiunga na Bayern Munich mwaka 1998.

Mwandishi:Aboubakary Liongo/DPA

Mhariri:Othman Miradji