Schumacher kustaafu Formula 1 | Michezo | DW | 23.11.2012
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Schumacher kustaafu Formula 1

Bingwa wa ulimwengu Sebastian Vettel amemmiminia sifa Michael Schumacher kuwa shujaa wake na aliyempa motisha wakati dereva huyo Mjerumani akijiandaa kushiriki mashindano yake ya mwisho kabisa katika taaluma yake

SINGAPORE - SEPTEMBER 23: Michael Schumacher of Germany and Mercedes GP retires early after crashing into the back of Jean-Eric Vergne of France and Scuderia Toro Rosso during the Singapore Formula One Grand Prix at the Marina Bay Street Circuit on September 23, 2012 in Singapore, Singapore. (Photo by Robert Cianflone/Getty Images)

Michael Schumacher Formel 1 Deutschland Rennfahrer

Schumacher ataendesha gari la Formula One kwa mara ya mwisho Jumapili hii katika mkondo wa Brazil Grand Prix. Schumacher anashikilia rekodi karibu zote za Formula One, ikiwa ni pamoja na ushindi 91 wa Grand Prix na kupata nafasi za kwanza 68 pamoja na mataji saba ya ubingwa wa F1 akiwa na timu za Benetton na Ferrari. Awali baada ya kustaafu mwishoni mwa mwaka wa 2006, alirejea tena katika mwaka wa 2010 na timu ya Merecedes, lakini katika awamu yake ya pili katika mashindano ya F1 hajaweza kuongeza mataji mengine na nafasi yake itachukuliwa msimu ujao na Lewis Hamilton. Mkufunzi wa timu ya taifa ya Ujerumani Joachim Loew anasema Schumacher ni jina maarufu kispoto kote ulimwenguni siyo tu nyumbani Ujerumani. Mafanikio yake katika F1 yanajieleza yenyewe na kamwe hayatasahaulika.

Sebastian Vettel amemsifu Michael Schumacher kwa kuwa mwelekezi

Sebastian Vettel amemsifu Michael Schumacher kwa kuwa mwelekezi

Nahodha wa zamani wa timu ya taifa ya Ujerumani Michael Ballack anasema Schumacher ni mmoja wa wanaspoti maarufu katika miongo iliyopita. Pia familia ya F1 imemsifu dereva huyo huku Kiongozi wa Ferrari Stefano Domenicali akisema jina la Schumacher limehusishwa na takribani nusu ya ushindi wa timu yake na atasalia mioyoni mwa familia ya Ferrari. Rais wa Mercedes Ross Brawn ambaye amewahi kufanya kazi na Schumacher kwa muda mwingi wa taalum yake amesema mbio za kesho nchini Brazil zitakuwa na huzuni kwa kila mtu katika kikosi chao.

Benitez afurahia kazi ya Chelsea

Kaimu mkufunzi mpya wa Klabu ya Chelsea Rafael Benitez amesema changamoto ya kujaribu kushinda mataji matano msimu huu ilikuwa ni fursa kubwa kwake kukataa wakati aliporejea katika Ligi ya Premier Alhamisi wiki hii.

Mhispania huyo mwenye umri wa miaka 52, ambaye aliondoka Liverpool mwishoni mwa msimu wa 2009-2010 na kuchukua nafasi ya Roberto Di Matteo uwanjani Stamford Bridge, kwamba ana furaha kujiunga na Chelsea na haijalishi kama ni mkataabw a muda mfupi au muda mrefu. Cha muhimu anasema ni kushinda mechi baada ya nyingine na kisha kutwaa mataji...

Chelsea wanahitaji muujiza kufuzu katika Ligi ya Mabingwa

Chelsea wanahitaji muujiza kufuzu katika Ligi ya Mabingwa

Pamoja na Premier League, mabingwa hao wa Ulaya bado wanashiriki katika Ligi ya Mabingwa ijapokuwa wanachungulia kaburi na ni muujiza wakifuzu katika awamu ya mchujo. Pia wanashiriki katika Kombe la Shirikisho, huku harakati za kutetea kombe la FA zikianza mwezi Januari, mwezi mmoja baada ya kushiriki katika kinyang'Anyiro cha Kombe la Klabu Bingwa Ulimwenguni.

Maafisa wakuu wa soka ya Uingereza sasa wataanza kurkodi mawasiliano wakati wa mechi kufutia kesi iliyomkabili Refarii Mark Clattenburg. Wakuu wa waamuzi wanalenga kuepuka marudio ya tukio kama hilo, baada ya Clattenburg kuondolewa madai na Shirkisho la Soka Uingereza FA, kwamba alimtolea matamshi ya kibaguzi kuungo wa Chelsea Mnigeria John Obi Mikel, baada ya uchunguzi wa muda mrefu kukosa kupata ushahidi wa kuwepo makosa yoyote.

Kwa sasa maafisa wa mechi katika ligi ya Premier, waamuzi wasaidizi na afisa wa nne, wote wana vifaa vya kusikiliza na kuzungumza ili kuwasaidia kuwasiliana vyema wakati kuna makelele uwanjani, lakini mazungumzo yao awali hayajakuwa yakirekodiwa.

Wakati huo huo, refarii Mark Clattenburg atajitosa uwanjani tena kutekeleza majukumu yake kuanzia kesho atakapoongoza mechi kati ya Tottenham Hotspurs dhidi ya Westham, na kisha asimamie mchuano wa Jumatano kati ya Southampton na Norwich katika uwanja wa St.Mary's.

Mwandishi: Bruce Amani/DPA/AFP/Reuters

Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman