Schubert apewa mkataba wa kudumu Gladbach | Michezo | DW | 13.11.2015
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Michezo

Schubert apewa mkataba wa kudumu Gladbach

Baada ya wiki kadhaa za kumtafuta kocha mpya, Borussia Mönchengladbach imefanya kile kilionekana kutoepukika. Kaimu kocha ambaye amepata mafanikio tangu apewe majukumu, Andre Schubert amepewa mkataba wa kudumu

Gladbach imetangaza kuwa Schubert ataongoza timu hiyo hadi mwisho wa msimu wa 2016-2017. Schubert mwenye umri wa miaka

Schubert mwenye umri wa miaka 44 ambaye alikuwa kocha wa timu ya vijana wasiozidi umri wa miaka 23, alichukua usukani kutoka kwa Lucien Favre miezi miwili iliyopita baada ya timu kushindwa mechi zake tano za ligi. Chini ya Schubert, walishinda mechi sita zilizofuata na kutoka sare mara moja. Wapanda kutoka nafasi ya mkia hadi ya sita kwenye msimamo wa ligi.

Mkurugenzi wa michezo wa klabu hiyo Max Eberl amesema Schubert ameonyesha mafanikio tangu alipochukua usukani na hivyo wanaamini timu hiyo iko katika mikono salama.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA
Mhariri: Daniel Gakuba

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com