1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Schalke yamtafuta kocha mpya baada ya kumtimua Wagner

Bruce Amani
28 Septemba 2020

Baada ya kumuachisha kazi David Wagner Schalke wanamtafuta kocha mpya. Anayepigiwa upatu ni kocha wa zamani wa Augsburg Manuel Baum, ambaye ni kocha wa vijana katika shirikisho la kandanda Ujerumani – DFB

https://p.dw.com/p/3j7q6
Fußball Trainer David Wagner auf Schalke entlassen
Picha: MIS/imago images

Baada ya kumuachisha kazi David Wagner Schalke wanamtafuta kocha mpya. Anayepigiwa upatu ni kocha wa zamani wa Augsburg Manuel Baum, ambaye ni kocha wa vijana katika shirikisho la kandanda Ujerumani – DFB.

Majina mengine ni Ralf Rangnick aliyewahi kuifundisha Schalke mara mbili, kocha wa zamani wa Mainz Sandro Schwarz na Marc Wilmots koicha wa zamani wa timu ya taifa ya Ubelgiji na mchezaji wa zamani wa Schalke.

Schalke ilimuachisha kazi jana Wagner baada ya mwanzo mbaya kabisa wa msimu wa Bundesliga. Wamelishwa mabao 11 na kufunga moja pekee katika mechi zao mbili za ufunguzi. Kichapo cha 3 – 1 Jumamosi dhidi ya Werder Bremen kilifuatia kishindo cha 8 – 0 mikononi mwa Bayern. Ina maana Wagner ameongoza mechi 18 za mwisho bila ushindi.