Schalke yamsajili Choupo-Moting kutoka Mainz | Michezo | DW | 05.07.2014
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Schalke yamsajili Choupo-Moting kutoka Mainz

Klabu ya Schalke imemsajili mshambuliaji wa Cameroon Eric Maxim Choupo-Moting kutoka kwa hasimu wake wa Bundesliga Mainz. Mkataba wa nyota huyo katika klabnu ya Mainz ulikamilika mwishoni mwa msimu uliopita.

Schalke imesema katika taarifa kuwa mkataba wa Choupo-Moting mwenye umri wa miaka 25 amesaini mkataba utakamweka katika kabu hiyo hadi Juni 2017. Meneja Mkuu wa Schalke Horst Heldt amesema Mcameroon huyo anaweza kucheza katika nafasi kadhaa lakini wanapanga kumpa fursa ya kuyaongoza mashambulizi yao.

Chopo Moting ambaye ni mzaliwa wa Hamburg aliichezea Hamburg SV na kumaliza msimu mmoja katika klabu ya Nuremberg kwa mkopo kabla ya kujiunga na Mainz mwaka wa 2011. Alifunga magoli 20 na kutengeneza mengine saba katika mechi 74 alizochezea Mainz katika Bundesliga.

Aliwahi kuichezea timu ya Ujerumani ya wachezaji walio chini ya umri wa miaka 21 kabla ya kuamua kuichezea timu ya taifa ya Cameroon na akacheza pia katika Kombe la Dunia.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP