Schalke yaendelea kumwinda Sami Khedira | Michezo | DW | 02.05.2015
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Schalke yaendelea kumwinda Sami Khedira

Kiungo wa Ujerumani Sami Khedira anasalia kuwa mchezaji anayemulikwa sana wakati klabu ya Schalke ikijiandaa kufanya mabadiliko katika kikosi chacke kwa ajili ya msimu ujao.

Mwenyekiti wa bodi ya klabu hiyo ya Bundesliga Clemens Toennis amesema “kutakuwa na mabadiliko” wakati Schalke ikiwa na msimu ambao haijaweza kufuzu katika nafasi ya kucheza Ligi ya mabingwa msimu ujao.

Toennies hajatoa maelezo zaidi lakini amesisitiza kuwa Schalke inamtaka Khedira mwishoni mwa msimu huu wakati mkataba wake katika klabu ya Real Madrid utakapofikia kikomo, mradi tu makubaliano mazuri ya kifedha yatafikiwa na mchezaji huyo. Schalke iko katika nafasi ya tano kwenye msimamo wa ligi wakati kukisalia na mechi nne msimu kukamilika.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/AP/DPA/Reuters
Mhariri: Mohamed Daman