1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Schalke 04 bado matokeo ni mabaya

Sekione Kitojo
26 Septemba 2016

Schalke 04 yakubali kipigo mara tano mfululizo msimu huu, na kuanza vibaya kabisa msimu huu wa Bundesliga. FC Bayern na Dortmund bado zafukuzana, wakati RB Leipzig yaendelea kung'ara.

https://p.dw.com/p/2QboD
Fussball Bundesliga TSG 1899 Hoffenheim vs. FC Schalke 04
Wachezaji wa Schalke wakipambana na HoffenheimPicha: Getty Images/Bongarts/A. Scheuber

Schalke  04 imeshindwa  kwa  mara  ya  nne  kupata  ushindi  katika Bundesliga  msimu  huu  baada  ya  kupoteza  mchezo  wake  jana jumapili  dhidi  ya  Hoffenheim  kwa  mabao  2-1. Hoffenheim imepata  ushindi  wake  wa  kwanza  katika  msimu  huu  baada  ya sare  nne  mfululizo  wakati  Lukas  Rupp  alipofunga  bao  katika dakika  ya  41. Mapema  Andrej Kramaric  alisawazisha  bao lililofungwa  na  Eric Maxim Choupo-Moting katika  dakika  ya  nne kwa  Schalke.

Nahodha  wa Schalke Benedict  Howedes   alikuwa  na  haya  ya kusema:

 "Kwa kweli  tulianza  vizuri . Tulipata  bao  zuri  kabisa. Hata  hivyo baadaye  tulianza  kujilinda na  katika  hali  hii  hatukuwa  maini sana. Tunafungwa  mabao mengi  ambayo ni kwa  njia  rahisi  sna. Nashindwa  kuelewa , ni  vipi  tunaweza  kufungwa  mabao  kama hayo. Na  hapa  kwa  mara  nyingine  tena tumeshindwa mchezo ambao  hatukupaswa  kushindwa, na  hii  inauma  sana."

Fussball Bundesliga TSG 1899 Hoffenheim vs. FC Schalke 04
Mlinzi wa Schalke 04 Benedickt Hoewedes akipambana na Andrej Kramaric wa HoffenheimPicha: Getty Images/Bongarts/A. Scheuber

Mbali  ya  kupata  mapokezi  mabaya  mjini  Kolon , lakini  wageni katika  ligi  ya  Bundesliga  RB Leipzig walipata  sare  muhimu  kwao , wakati  timu  zote  hizo  zikibakia   bila  kushindwa  katika  mchezo wa  tano  wa  msimu  huu, baada  ya  kutoka  sare  kwa  bao 1-1.

Mashabiki  wa  FC Kolon  walilizuwia   basi  lililokuwa  likiwaleta wachezaji  wa  Leipzig na  mchezo  ulianza  dakika  15  baada  ya muda  uliopangwa. Leipzig inafadhiliwa  na  kampuni  ya  Austria inayotengeneza  kinywaji  baridi  cha  kutia  nguvu na  kuchipuka kutoka  katika  ligi  za  chini  hadi  katika  Bundesliga  msimu  huu. Mashabiki  wengi  wa  Bundesliga  hawafurahishwi  na  kikosi  hicho kutokana  na  mahusiano  yake  ya  kibiashara  na  kampuni  hiyo. Mchezaji aliyesainiwa msimu  huu  na  Leipzig ,  raia  wa  scottland Oliver Burke, alicheza  kwa  mara  ya  kwanza  na  alipachika  bao katika  dakika  ya  tano  ya  mchezo. Kolon walisawazisha   katika dakika  ya  25  kwa  bao  la  yuya Osako.

Huyu  hapa Marcel Sabitzer  wa  RB Leipzig .

Fussball Bundesliga TSG 1899 Hoffenheim vs. FC Schalke 04
Andrej Kramaric (kulia) wa Hoffenheim akishangiria bao lake dhidi ya Schalke 04Picha: Getty Images/Bongarts/A. Scheuber

"Nafikiri  katika  kipindi  cha  kwanza  tulianza  vizuri. Tuliweza kupata  bao. Na  baada  ya  hapo  tulicheza  vizuri. Lakini  Kolon waliweza  kurejesha  bao  haraka. Na  baada  ya  hapo  wwalicheza vizuri  pia. Katika  kipindi  cha  pili  timu  zote  hazikuweza  kucheza vizuri  kutokana  na  kuchoka  kwasababu  ya  michezo  mfululizo. Tulijaribu  kila  kitu, lakini  tunafuraha  kupata  pointi  moja  kutoka hapa."

Hadi  sasa  Bayern Munich  inaongoza  Bundesliga  kwa  kuwa  na pointi 15 , ambapo imeshinda  michezo  yake  yote. Inafuatiwa  na Borussia  Dortmund  katika  nafasi  ya  pili  ikiwa   na  pointi 12, pamoja  na  FC Kolon  ambayo  ina  pointi 11 katika  nafasi ya  tatu.

Kibarua chaota majani

Bayern  iliishinda  Hamburg SV  kwa  taabu  siku  ya  Jumamosi  kwa bao  1-0  lililofungwa  katika  dakika  ya  91  na  Joshua  Kimmich, lakini   hali  ya ukakamavu  iliyooneshwa  na  Hamburg  haikuweza  kumuokoa kocha  Bruno  Labbadia  kung'olewa  katika  kiti  chake  kilichokuwa kinalegalega.

Markus Gisdol
Kocha mpya wa Hamburg SV Markus Gisdol Picha: picture-Alliance/dpa/F. Gambarini

 Ni  mara  ya  pili  katika  msimu  huu  kushuhudia  kocha  kibarua kikiota  majani, ambapo  baada  ya  Werder  Bremen  kuachana  na kocha  wake  Viktor Skriptnik  wiki moja  iliyopita, wiki  hii  Hamburg SV  iliachana  na  kocha  wake Bruno Labbadia Jana  Jumapili  jioni na  kumtaja  mrithi  wake  kuwa  ni  kocha  wa  zamani  wa Hoffenheim  Markus Gisdol na  kusaini  mkatab  hadi  Julai 2017. Gisdol  mwenye  umri  wa  miaka  47  pamoja  na  kocha  wake msaidizi  Frank Fröhling  na  Frank Kaspari  wanatarajiwa  kuanza rasmi  kazi  ya  kuifunza  Hamburg  leo  jioni.

Gisdol  ambaye  alifanyakazi  na  Hoffenheim  tangu  Aprili  2 , 2013 hadi  Oktoba 26 , 2015 , alifanikiwa  kuwaweka  Kevin Volland, Sebastian rudy  na  Roberto Firmino  ambaye  hivi  sasa  yuko  na Liverpool  kuwa  wachezaji  wa  timu  za  taifa  za  Ujerumani  na Brazil.

Matarajio  ya  Hamburg  kwa  Gisdol ni  kuiondoa  timu  hiyo  kutoka mkiano  mwa  ligi, na  pia  kuipa  makali  safu  ya  ushambuliaji ambapo wachezaji  kama  Boby Wood  na  Filip  Kostic wameshindwa  kuzifumania  nyavu  za  maadui  chini  ya  uongozi wa  Labbadia.

Katika  ligi  ya  Uingereza  Premier League , Manchester  United iliondoka  kifua  mbele  mbele  ya  mabingwa  watetezi  Leicester City  siku  ya  Jumamosi  kwa  kuizaba  mabao  4-1  ambapo kocha wa  Jose Mourinho  aliweka  kando kutokuwapo  uwanjani  kwa Wayne Rooney  kuwa  ndio  sababu  ya  kikosi  chake  kufanikiwa kutandaza  kandanda  safi  siku  hiyo na  kuudhibiti  mchezo. Mourinho  alisema.

"Leo ilikuwa  muhimu  kuwa  na  watu  wenye  kasi  uwanjani kupambana  na  timu  ambayo  inashambulia kwa  kushitukiza  moja kwa  moja  kuanzia  katika  robo  ya  eneo  lao  wakipiga  mipira  ya mbali  na  wachezaji  kufikia  mara  mpira  unapotua upande  wa  pili. Kwa  hiyo  tumebadilisha  timu kucheza  dhidi  ya  Leicester kwa kuwa  na  uwezo  maalum  walionao".

Jose Mourinho Manager Manchester United
Kocha jose Mourinho wa Manchester UnitedPicha: picture-alliance/dpa/M.Rickett

Chelsea  ilikiona  cha  mtema  kuni  baada  ya  kufanya  makosa makubwa  kila  mara  katika  ulinzi  na  kuzabwa  mabao  3-0  na Arsenal London wakati  kikosi  cha  mzee  Arsene Wenger  kilifikisha mwisho  ukame  wa  mabao  katika  michezo  sita  ya  ligi  dhidi  ya majirani  zao  hao  mjini  London  kwa  kupachika  mabao  3  katika kipindi  cha  kwanza.

Liverpool  haijatawazwa  mabingwa  wa  England  tangu  mwaka 1990 na  mchezo  dhidi  ya  Hull City  umejionesha  kwamba  timu hiyo  inarejea  katika  safu  yake  tena.

Manchester  City  wanaongoza  ligi  hiyo  kwa  kushinda  michezo yake  yote  sita  na  Jumamosi  iliizaba Swansea  City  kwa  mabao 3-1.

Bayern Munich, Borussia Dortmund  na  Borussia Moenchengladbach  zinakabiliana  na  changamoto  kutoka Uhispania  katika  Champions League  wiki  hii wakati  Bundesliga inajipima  nguvu  dhidi  ya  vilabu  kutoka  La  Liga , Premira Division.

Borussia  Dortmund  itakuwa  wenyeji  wa  mabingwa  watetezi  Real Madrid  kesho  Jumanne wakati  siku  ya  Jumatano  itakuwa  zamu ya  Gladbach  kuoneshana  kazi  na  FC Barcelona  na  Bayern Munich inajaribu  kulipa  kisasi  cha  kuondolewa  katika  nusu  fainali mwaka 2016  na  atletico  Madrid.

Deutschland Dortmund - 1. Bundesliga - Borussia Dortmund gegen SC Freiburg
Borussia Dortmund iliyoanza vizuri msimu huu wa Bundesliga inakabana koo na Real Madrid katika Champions LeaguePicha: picture-alliance/dpa/I. Fassbender

Mara  hii Bayern Munich  iko  chini  ya  ukufunzi  wa  kocha  mpya Carlo Ancelotti  ambaye  ameonesha  uwezo  mkubwa  kwa kushinda  hadi  sasa  michezo  yote  mitano  katika  Bundesliga.

"Tumecheza  na  timu  za  Uhispania  katika  kipindi  cha  miaka mitatu  iliyopita  na  kila  wakati  tulishindwa", amesema  mwenyekiti wa  Bayern Karl-Heinz Rummenigge. Tukiwa  na  kocha  Carlo Ancelotti tunataka  kuwaonesha  Atletico Madrid  kwamba  tunaweza kushinda  hata  pointi  moja  ama  tatu  kwao." ameongeza Rummenigge.

Michezo  mingine ni kati  ya  Monaco  ikikwaana  na  Bayer Leverkusen ya  Ujerumani , CSKA Moscow  ikioneshana  kazi  na  Tottenham Hotspurs  ya  Uingereza , Sporting Lisbon ina  miadi  nyumbani  na Legia  Warsaw, Club Brugge  inasafiri kwenda  kwa  FC Copenhagen  ya  Denmark , wakati  Leicester  City  mabingwa  wa Uingereza  wako  nyumbani  wakiisubiri FC Porto  ya  Ureno.

Champions League Afrika

Na  katika  bara  la  Afrika  Zamalek  ya  Misri  ilipata  kipigo  cha mbwa  mwizi  cha  mabao  5-2 mbele  ya  wababe  wa  Morocco Wydad Casablanca siku  ya  Jumatatu  lakini  walihimili kishindo hicho  na  kufanikiwa  kufuzu  kukutana  na Mamelodi Sundowns  ya Afrika  kusini   katika  fainali  ya  kombe  la  Champions League barani  Afrika.

Mabingwa  hao  mara  tano   wa  Afrika  walishinda  mchezo  wao wa  mkondo  wa  kwanza  wa  nusu  fainali  kwa  mabao 4-0  mjini Alexandia  mwishoni  mwa  juma  lililopita na  kufanikiwa  kujipenyeza katika  fainali  kwa  jumla  ya  mabao 6-5.

Bundesliga FC Bayern München - Hertha BSC Berlin
Kikosi cha wachezaji wa Bayern Munich kinajitayarisha kupambana na Atletico Madrid katika Champions LeaguePicha: picture-alliance/dpa/A. Gebert

Ikijaribu  kuwa  timu  ya  kwanza  kufuta  kipigo  cha  mabao  manne katika  nusu  fainali, ya   kombe  la  champions league  barani  Afrika , Wydad  ilikuwa  inaongoza  kwa  mabao 5-1 dakika  26  kabla  ya mchezo  kumalizika lakini  ilijikuta  ikiwa  nyuma  kwa  sheria  ya mabao  ya  ugenini.

Nayo TP mazembe  ya  jamhuri  ya  kidemokrasi  ya  Congo  imefikia fainali  ya  kombe  la  shirikisho  barani  Afrika   jana  jumapili  baada ya  kutoka  suluhu  na  wageni  wao  kutoka  Tunisia  Etoile Sahel bila  kufungana  katika  mchezo  wa  mkondo  wa  pili  wa  nusu fainali.

Na  katika  riadha :

Kenenisa  Bekele  wa  Ethiopia  alimpita  Wilson kipsang  wa  Kenya aliyekuwa  akishikilia  rekodi  ya  dunia  ya  mbio  hizo , kilomita moja  kabla  ya  kufikia  mwisho  na  kushinda  mbio  za  Marathon mjini  Berlin  jana  Jumapili. Bingwa  mara  tatu   wa  Olimpiki  Bekele alishindwa  hata  hivyo  kuifikia  rekodi  ya  dunia kwa  sekunde  sita wakati  akimaliza  kwa  kutumia  saa  mbili  dakika  3  na  sekunde 3, akiondoa  dakika  mbili  katika  rekodi  yake  binafsi.

Evans Chebet  wa  Kenya  alikuwa  wa  tatu  kwa  kukimbia  saa 2 dakika  05  na  sekunde 31.

10.000m-Olympiasieger Kenenisa Bekele
Kenenisa Bekele wa Ethiopia alikuwa mshindi wa Berlin Marathon Jumapili (25.09.2016)Picha: AP

Nalo  pambano  la  ngumi  la  marudio  katika  Tyson Fury  na Wladimir  Klitschko  kwa  ajili  ya  ubingwa  wa  dunia  wa  uzito  wa juu  umefutwa  kwa  mara  ya   pili. Kampuni  inayofanya  masuala ya  kiutawala  ya  Fury , Hennessy  Sports, imesema  siku  ya Ijumaa  kwamba  mwanamasumbwi  huyo  kutoka  Uingereza , ameelezwa  kwamba  hayuko  sawa  kiafya   kuweza  kupigana na pambano  la  Oktoba  29 mjini  Manchester , halitafanyika.

 

Mwandishi: Sekione  Kitojo / ape /  rtre / afpe / dpae

Mhariri: Yusuf , Saumu