1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Saudi Arabia yatishia kulipiza kisasi

Isaac Gamba
15 Oktoba 2018

Saudi Arabia imetishia kujibu vikali vikwazo vyoyote vitakavyotangazwa dhidi yake baada ya rais Donald Trump kusema taifa hilo linastahili kuadhibiwa kama itabainika kuhusika na suala la Khashoggi.

https://p.dw.com/p/36YIH
Saudi Arabien |  Prince Mohammed bin Salman "Vision 2030"
Picha: Getty Images/AFP/F. Nureldine

 

Ujerumani, Ufaransa na Uingereza kwa pamoja zimetoa wito zikitaka uchunguzi wa kina ufanyike kuhusiana na kutoweka kwa Jamal Khashoggi hiyo ikiwa ni kwa mibu wa taarifa iliyosainiwa na waziri wa mambo ya nje wa Uingereza Jeremy Hunt , Jean-Yves Le Drian wa Ufaransa na waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Heiko Maas.

Ufalme wa Saudi Arabia unasema tuhuma dhidi yake kuhusiana na suala la Khashoggi hazina msingi. Hata hivyo ufalme huo haujatoa ushahidi unao onesha mwandishi huyo wa habari  ambaye amekuwa  akimkosoa mfalme wa Saudia Mohammed bin Salman kama  aliondoka katika ubalozi wa mdogo wa Saudi Arabia mjini Istanbul.

 

Ikulu ya Marekani imepuuza  vitisho vya Saudi Arabia kwamba huenda ikalipiza kisasi kwa hatua yoyote ya Marekani kuiadhibu kichumi falme hiyo, kuhusiana na tuhuma za mauaji ya mwandishi Khashoggi, huku ikitoa wito wa uchunguzi ulio wazi kuhusiana na kutoweka kwake.

Maseneta wawili wa chama cha Republican, wamesema bunge la Marekani liko tayari kuchukua hatua ikiwa ni pamoja na uwezekano wa kuzuwia uauzaji silaha kwa Saudi Arabia.

 Mshauri wa masuala sya uchumi  wa Ikulu ya White house Larry Kudlow alikataa kutabiri  kile kitakachofanywa na Rais Donald Trump baada ya kuahidi hatua kali wakati wa mahojiano ya dakika 60 hapa Jumapili, ikiwa Marekani itakuwa na ushahidi kwamba  Khashoggi  aliuwawa  ndani ya ubalozi mdogo wa Saudi Arabia  mjini Istanbul.

Akizungumza katika mahojiano yaliyoendeshwa na kituo cha matangazo cha CBS rais Donald Trump alisema Marekani italifuatilia kwa kina suala hilo na kutakuwa na adhabu kali kwa anayehusika.

Donald Trump
Rais wa Marekani, Donald TrumpPicha: Imago/MediaPunch

Kwa upande mwingine Trump amesema  Marekani itakuwa inajiadhibu yenyewe iwapo itasitisha mauzo ya silaha kwa Saudi Arabia kwani silaha hizo zinauzwa na  makampuni ya Marekani na hata kama Saudi Arabia haitanunua silaha kutoka makampuni ya  Marekani  basi itanunua kwingine.

Khashogi anayeandikia pia gazeti la Washington Post alitoweka Oktoba 2  baada ya kuingia ubalozi mdogo wa Saudi Arabia mjini Istanbul.

Tayari viongozi wa kimataifa wanaohusika na masuala ya kibiashara wameanza kujiondoa kushiriki kongamano lijalo la uwekezaji katika taifa hilo la kifalme lililopewa jina la "kongamano la Davos jangwani"

Hayo yanajiri mnamo wakati biashara ya kubadilisha fedha ikiporomoka hadi kufikia kiwango cha alama zaidi ya 500 kabla ya kufikia alama 264 au baadaye kufikia zaidi ya asilimia 4.

Issam Kassabieh  mchambuzi wa masuala ya fedha  katika kampuni moja ya masuala ya fedha  iliyo na makao yake mjini Dubai anasema suala kama hili lazima litaogopesha wawekezaji  kwani  hawaoni kama wako salama nchini Saudi Arabia kwa hiyo ni rahisi kuondoa uwekezaji wao.

Mwandishi: Isaac Gamba/APE

Mhariri :Caro Robi