1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Saudi Arabia kuhudhuria mkutano kuhusu amani ya Mashariki ya Kati

24 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CSgX

Waziri wa mashauri ya kigeni wa Saudi Arabia, mwanamfalme Saud al Faisal, amesema Saudi Arabia itahudhuria mkutano unaolenga kuyafufua mazungumzo ya kuumaliza mgogoro baina ya Israel na Palestina, utakaofanyika huko Annapolis katika jimbo la Maryland, nchini Marekani.

Kushiriki kwa Saudi Arabia katika mkutano huo kutamuongezea nguvu rais wa mamlaka ya Palestina, Mahmoud Abbas, kuweza kufikia makubaliano na kumsaidia waziri mkuu wa Israel, Ehud Olmert, kuyawasilisha makubaliano hayo kwa Waisraeli ili wawe na amani na nchi za kiarabu.

Marekani imeukaribisha uamuzi wa Saudi Arabia kuhudhuria mkutano wa mjini Annapolis, na kuzitolea mwito nchini nyingine za kiarabu pia zihudhurie. Syria imesema Marekani imekubali kuliingiza swala la ardhi ya milima ya Gholan katika ajenda ya mkutano huo.

Waziri wa mashauri ya kigeni wa Syria, Walid al Moualem, amesema Syria itaamua ikiwa ihudhurie mkutano wa Annapolis, mara tu itakapopokea ratiba ya mkutano huo.