Sarkozy na Merkel wakubaliana kuhusu msaada wa Ugiriki | Matukio ya Kisiasa | DW | 18.06.2011
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Sarkozy na Merkel wakubaliana kuhusu msaada wa Ugiriki

Viongozi wa Ufaransa na Ujerumani wamekubaliana kuhusu mpango wa pili wa kuipatia Ugiriki msaada wa fedha ili kuinusuru na madeni, licha ya tofauti zao.

default

Rais Nicolas Sarkozy wa Ufaransa na Kansela Angela Merkel wa Ujerumani

Mpango huo unahusisha sekta binafsi kuchangia mfuko wa kuziokoa nchi zisifilisike kwa njia ya mikopo ya hiari.

Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel amekuwa akishinikiza wawekezaji binafsi kuchangia hadi theluthi moja ya msaada huo mpya, lakini alikubali kuafikiana na Rais wa Ufaransa, Nicolas Sarkozy. Thamani ya sarafu ya Euro ilipanda kufuatia mkutano huo mjini Berlin.

Inatathminiwa kuwa Ugiriki inahitaji msaada wa Euro bilioni 80 hadi 120 ili kuepuka kufilisika, baada ya msaada wa mwaka uliopita na hatua kali za mageuzi kushindwa kurejesha imani ya masoko.

Mkutano wa viongozi hao wawili mjini Berlin utafuatiwa na mkutano wa kilele wa Umoja wa Ulaya utakaofanyika wiki ijayo mjini Brussels.

Mwandishi: Grace Patricia Kabogo (RTRE,AFP)
Mhariri: Prema Martin

 • Tarehe 18.06.2011
 • Mwandishi Kabogo Grace Patricla
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/11eaR
 • Tarehe 18.06.2011
 • Mwandishi Kabogo Grace Patricla
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/11eaR

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com