1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Sarkozy likizo Misri

23 Desemba 2007

---

https://p.dw.com/p/CfWB

CAIRO:

Rais Nicolas Sarkozy wa Ufaransa anatarajiwa kuwasili Sharm el Sheikh nchini Misri hapo kesho kwa likizo ya X-masi.

Ziara yake itajumuisha matembezi huko Luxor na kuwa na majadiliano wazi na waandishi na wasomi wa Misri.

Haifahamiki iwapo rais wa Ufaransa atafuatana katika likizo yake hiyo na mpenzi wake mpya alievumishiwa -muimbaji wa asili kifaransa na kitaliana Carla Bruni.