SAO PAULO : Wataka kufungwa kwa uwanja wa ndege | Habari za Ulimwengu | DW | 20.07.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

SAO PAULO : Wataka kufungwa kwa uwanja wa ndege

Waendesha mashtaka Brazil wanataka kuchukuwa hatua za kuufunga uwanja wa ndege wa Congohas wakati wachunguzi wakichunguza ajali ya ndege iliotokea Jumatano na kuuwa takriban watu 189.

Ukanda wa filamu wa camera za uwanja wa ndege umeonyesha jinsi ndege hiyo ya shirika la ndege la Tam ilivyotuwa katika mwendo wa kasi mno kwenye njia ya kutulia ndege na baadae kuyumba na kujibamiza kwenye kituo cha mizigo na bohari la mafuta ambapo iliripuka.

Rubani mmoja amesema njia za kurukia na kutulia ndege zilizonyeshewa na mvua huteleza kama sabuni wakati chama cha marubani wa kimataifa kikidai kuwepo kwa hatua bora zaidi za usalama kwa mashirika ya ndege kwenye uwanja huo wa safari za ndani ya nchi ulio muhimu kabisa nchini Brazil.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com