SANAA:Wahispania saba wauawa katika shambulizi la kigaidi | Habari za Ulimwengu | DW | 03.07.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

SANAA:Wahispania saba wauawa katika shambulizi la kigaidi

Watalii saba wa Uhispania na raia wawili wa Yemen wameuawa katika shambulizi la kigaidi la kujitoa mhanga huko Yemen.

Wizara ya mambo ya nje ya Uhispania imesema kuwa watu wengine wawili walijeruhiwa katika shambulizi.

Wizara ya mambo ya ndani ya Yemen imewalaumu wanachama wa kundi la Al Qaida kwa kuhusika na shambulizi hilo lililotokea katika mji wa Marib kiasi cha kilomita 150 kaskazini mwa mji mkuu wa Yemen Sanaa.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com