SAN JOSE: Mtu mwenye silaha ateka watu katika ubalozi wa Russia nchini Costa Rica. | Habari za Ulimwengu | DW | 12.05.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

SAN JOSE: Mtu mwenye silaha ateka watu katika ubalozi wa Russia nchini Costa Rica.

Mtu mwenye silaha aliyekuwa amewateka nyara watu katika ubalozi wa Russia nchini Costa Rica, amejisalimisha kwa polisi kiasi saa nne tangu alipoingia humo ubalozini.

Hakuna mtu aliyeumizwa wakati wa kizaazaa hicho.

Hapo awali maafisa wa serikali walikuwa wamesema mtu mmoja alikuwa amewateka nyara watu wanane kisha baada ya muda mfupi akawaachilia mateka watano.

Hata hivyo balozi wa Russia nchini humo, Valery Nikolayenko aliwaambia waandishi wa habari kwamba yeye pamoja na maafisa wengine watatu walikuwa wamebaki ubalozini humo wakijaribu kumbembeleza mteka nyara huyo awaachie huru mateka wake.

Vyombo vya habari vya Costa Rica viliarifu kwamba mtu huyo hao ni raia wa Urusi ya zamani mwenye umri wa miaka kati ya kumi na saba na ishirini.

Polisi walikuwa wamelizingira eneo la ubalozi huo ambao umo kwenye sehemu ya makazi.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com