1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
AfyaRwanda

Rwanda yazuia matumizi ya dawa inayoshukiwa kuwa na sumu

15 Aprili 2024

Mamlaka ya kudhibiti viwango vya dawa Rwanda, imeiondowa dawa ya kikohozi ya watoto ya kampuni ya Johnson & Johnson kutokana na wasiwasi wa kuwa na kiambata cha sumu.

https://p.dw.com/p/4eoJg
Symbolfoto I Hustensaft
Picha: Bilderbox/picture alliance

Hatua hiyo ya tahadhari  imechukuliwa baada ya Nigeria kusema vipimo vya maabara ya dawa hiyo ya maji vilionyesha kiwango kikubwa cha aina ya kemikali ya diethylene glycol inayohusishwa na vifo vya watoto nchini Gambia, Uzbekistan na Cameroon tangu mwaka 2022.

Rwanda imeungana na Kenya, Afrika Kusini na Nigeria kurejesha dawa hizo zinazotumika  kutibu kikohozi, homa kali na mzio kwa watoto.

Dawa zilizorejeshwa zilitengenezwa na kampuni ya J&J nchini Afrika Kusini mwezi Mei mwaka 2021 kabla ya kuuzwa kwa kampuni ya Kenvue ambayo sasa inamiliki chapa ya Benylin Paediatric syrup. Kenvue imesema inafanya uchunguzi wake na kufanya kazi na taasisi za afya kuangalia hatua inayoweza kuchukua.