1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rwanda yawasaidia watoto walioathirika na virusi vya HIV

Saumu Ramadhani Yusuf12 Novemba 2010

Watoto kiasi cha 200,000 wanaishi na Virusi vya HIV nchini humo

https://p.dw.com/p/Q3ge
Shirika la UNICEF laisaidia Rwanda katika kuwapa msaada watoto wenye virusi vya HIVPicha: AP

Takriban watoto 30 wenye umri kati ya miaka 12 hadi 18 husubiri katika chumba kilichojaa watu katika hospitali ya Kibagabaga kupata maelezo ya matumizi ya madawa ya kurefusha uhai wa watu walioathiriwa na vijidudu vya HIV. Mohamed Dahman anasimulia mahitaji ya msaada zaidi kwa watoto walioathirika na virusi vya HIV nchini Rwanda.

Watoto hao ni miongoni mwa watoto 200,000 walioathiriwa na virusi vya HIV ambao wanafaidika na msaada wa kijamii na matibabu kutoka serikali ya Rwanda na washirika wake wa maendeleo.

Antoinette Murebwariye  muuguzi katiika kituo kimoja cha matibabu anasema baadhi ya watoto hao hawawezi kwenda hata kwa madktari kuelezea mateso yao kwa sababu yumkini wakawa na hofu na baadhi yao huhisi kuwa na hatia nsa wengi wa watoto hao huwa mayatima wa HIV.. Muuguzi huyo anasema wao ndio wazazi wao.

Tunga ambaye sio jina lake halisi ni mvulana mwenye umri wa miaka 13 kutoka Samuduha  mojawapo ya kitongoji cha kimaskini kabisa nchini Kigali. Anasema wazazi wake walikufa kutokana na UKIMWI hapo mwaka 2008 wakati alipokuwa na umri wa miaka sita. Tunga mwenyewe alikuwa hajuwi iwapo alikuwa ana virusi vya HIV wasi wasi wake mkubwa ulikuwa ni kuwahudumia ndugu zake wadogo wawili wa kiume.

Kituo cha matibabu ya watoto katika hospitali ya Kibagabaga huona wagonjwa 30 kila siku kwa ajili ya uchunguzi, ushauri nasaha na matibabu.Kuna watoto 870 wanaopatiwa matibabu katika kituo hicho na 55 kati yao hupatiwa matibaba ya kurefusha maisha ya vidonge vya anti- retroviral.

Lakini inasemekana kwamba watoto wengi waliathiriwa na virusi vya HIV wanatoka katika familia za kimaskini zilio rahisi kuathirika inakuwa vigumu kwao wao kutumia madawa hayo kutokana na njaa.

Hospitali ya Kibagabaga hutowa bure ushauri nasaha na kuwafanyia uchunguzi mayatima wa UKIMWI na kwa kijana Tunga haina tatizo katika kufanyiwa uchunguzi huo.

Anasema kufanya uchunguzi wa virusi vya HIV ilikuwa rahisi kwake yeye lakini wakati alipoambiwa kwamba alikuwa na virusi vya HIV ilikuwa ni habari nyengine kwani wakati alipoambiwa kwa mara ya kwanza kwamba alikuwa alikuwa na virusi hivyo alihisi kuwa ni kama adhabu kwa kitu fulani alichokifanya.

Lakini Tunga alikuwa na bahati kupata msaada kutoka duru kadhaa. Yeye na kaka zake wawili wadogo waniashi katika nyumba ambayo imejengwa na shirika lisilo la kiserikali la ndani ya nchi hapo mwaka 2009 baada ya ndugu hao watatu kugundulikana kuwa hawana nyumba.

Familia hiyo ndogo pia hupata msaada katika Mpango wa Familia ambao ni msaada wa kijamii na matibabu ambaoserikali inautekeleza kwa ajili ya watu wenye UKIMWI na HIV. Mpango huo unaoungwa mkono na UNICEF huzipatia familia zulizoathiriwa na virusi vya HIV na UIKIMWI matibabu na ushauri nasaha,uzazi wa majira na msaada wa lishe pamoja na mradi wa kuzalisha mapato.

Familia zenye kuongozwa na watoto huapatiwa msaada kwa kuluipiwa ada z shule na sare za shule pamoja na chakula cha kila mwezi.

Wakati wazazi wake walipokufa  Tunga alipoteza matumaini ya kuishi lakini kwa msaada alioupata ameweza kuwaelimisha wadogo zake na hawakulazimika kuacha shule.

Hata hivyo inaelezwa kwamba msaada wa afya kwa watoto walioathirika na virusi vya HIV unaotolewa na serikali ya Rwanda bado msaada zaidi unahitajika.

Watoto wengi wanaoishi katika maeneo ya kimaskini hawatambui juu ya kupatikana kwa huduma hizo za bure. Mayatima wa UKIMWI na watoto wanaoishi na virusi vya HIV mara nyingi hukosa msaada wa hali na hutengwa na jamii inayowazunguka kutokana na unyanyapaa.

Mwandishi: Dahman, Mohamed/IPS

Mhariri: Josephat Charo