Russia yapendekeza kutumia kituo cha pamoja na Marekani. | Matukio ya Kisiasa | DW | 08.06.2007
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Russia yapendekeza kutumia kituo cha pamoja na Marekani.

Rais wa Russia Vladimir Putin ametoa wito wa kuwa na kituo cha pamoja kati ya nchi yake na Marekani cha kutambua ujio wa mashambulizi ya makombora katika pendekezo ambalo halikutarajiwa la kutanzua mzozo baina ya mataifa hayo mawili.

Urafiki wa mashaka, rais Bush akishikana mkono na rais Putin wa Russia katika mkutano wa G8 nchini Ujerumani.

Urafiki wa mashaka, rais Bush akishikana mkono na rais Putin wa Russia katika mkutano wa G8 nchini Ujerumani.

Putin amependekeza kwa rais George W. Bush matumizi ya pamoja ya kituo cha rada cha Russia ikiwa kama ni mpango mbadala wa ulinzi wa makombora wa Marekani katikati ya bara la Ulaya.

Russia imeghabika na kuupinga mpango huo wa Marekani wa kuweka mfumo wa ulinzi wa makombora nchini Poland na jamhuri ya Chek na Putin ametishia kurejea katika enzi za sera ya vita baridi yenye kulenga makombora ya Russia kuelekea Ulaya, iwapo mfumo huo utawekwa.

Putin amesema kuwa mpango wa pamoja wa kuwa na kituo kimoja utaondoa haja na utaruhusu mataifa hayo mawili kutobadilisha sera zao kuhusiana na hatua ya kutoyalenga makombora yao kwa mwengine.

Putin na Bush walikutana jana Alhamis pembezoni mwa mkutano wa kundi la mataifa ya G8 mjini Heiligendamm, Ujerumani katika juhudi za kuuokoa uhusiano wao ambao ulifikia katika hatua ya chini ya enzi kabla ya vita baridi. Bush amesema kuwa pendekezo hilo la Russia si baya na kupendekeza binafsi kuwa wataalamu kutoka mataifa haya mawili wachunguze uwezekano huo.

O-Ton Bush

Bush binafsi amewaambia waandishi wa habari kuwa viongozi hao wawili wataendeleza mkakati wa mazungumzo katika mazungumzo yatakayofanyika Marekani mapema Julai mwaka huu.

Putin amesema kuwa amezungumza siku ya Jumatano na rais wa Azerbaijan, Ilham Aliyev , ambaye amekubali kuwa kituo cha kijeshi cha Gobalin kilichokodishwa na Russia kinaweza pia kutumiwa kwa pamoja na Marekani.

Russia inasema kuwa ngao hiyo dhidi ya makombora inayopendekezwa na Marekani katika eneo la Ulaya inailenga binafsi, wakati Marekani inasisitiza kuwa mfumo wake huo ni ulinzi dhidi ya mashambulizi kutoka Iran ama Korea ya kaskazini.

O-Ton Bush

Tunamsimamo mmoja kuhusu vitisho lakini kuna tofauti juu ya njia za kupambana na vitisho hivi, Putin amesema baada ya mazungumzo na Bush.

Putin anadai kuwa majeshi ya Russia na Marekani yanaweza kutambua jaribio lolote la makombora ya masafa marefu litakalofanywa na Iran na baadaye watakuwa na muda hadi miaka mitano kuweka kituo cha pamoja kabla ya kuwapo na kitisho kikubwa.

 • Tarehe 08.06.2007
 • Mwandishi Sekione Kitojo
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/CHD0
 • Tarehe 08.06.2007
 • Mwandishi Sekione Kitojo
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/CHD0

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com