″Rushwa yazorotesha uchumi duniani″ | Matukio ya Kisiasa | DW | 05.12.2012
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Kisiasa

"Rushwa yazorotesha uchumi duniani"

Ripoti ya mwaka huu ya shirika la kimataifa linalopambana na ufisadi duniani, Transparency Intenational, inasema rushwa imechochea kwa kiasi fulani mgogoro wa uchumi duniani, huku Somalia na Korea Kaskazini zikiongoza.

A European Union left and the Greek flag wave above the ancient Parthenon temple, at the Acropolis Hill, in Athens on Monday, July 11, 2011.Greece's Socialist government on Monday named a five-member committee to head a euro50 billion ($71.2 billion) privatization program aimed at easing the country's euro340 billion ($484.2 billion) national debt. (Foto:Petros Giannakouris/AP/dapd)

Ugiriki yaathirika kwa Rushwa

Pamoja na kuwepo kwa kampeni mbalimbali na katika maeneo tofauti duniani dhidi ya ufisadi, lakini faharasa ya rushwa ya shirika la Transparency International inaonesha kuwa theluthi mbili kati ya mataifa 176 yamepata chini ya asilimia 50. Hiyo inamaanisha zimekithiri sana kwa rushwa.

Ripoti hiyo inaeleza kwamba kukithiri kwa vitendo vya ufisadi ndiko kulikochochea baadhi ya viongozi kulazimishwa kuondoka madarakani mwaka jana, ingawa bado kiwango chake kimeendelea kuwa cha juu zaidi katika mataifa mengi.

Mataifa matatu bora barani Ulaya

Greece's PM Antonis Samaras waits for visiting Luxembourg's PM and Eurogroup Chairman Jean-Claude Juncker before their meeting in Athens (Foto: Reuters) / Eingestellt von wa

Waziri Mkuu wa Ugiriki Antonis Samaras

Kwa mara nyingine, Dernmark, Finland na New Zealand zimekuwa na rikodi nzuri kwa mujibu wa Transparency International wakati Afghanstan, Korea Kasikazini na Somalia zikisalia mkiani katika kadhia ya rushwa.

Kwa kuzingitia kipimo kinachoanisha sifuri - kama kiwango kibaya zaidi cha rushwa - mpaka 100 - ikiwa ndiyo rikodi nzuri kabisa, Dernmark, Finland na New Zealand zimefungana kwa kupata alama 90. Lakini Afghanstan, Korea Kaskazini na Somalia kila moja imepata alama 8.

Hali ilivyo katika mataifa ya Kiarabu

Pamoja na hayo, ripoti hiyo imeonesha kumekuwa na mafanikio kidogo sana katika mataifa ya Kiarabu yaliyokumbwa na vuguvugu la kisiasa. Mataifa hayo ni pamoja na Misri na maeneo mengine ya Mashariki ya Kati.

Mataifa ambayo ni kiini cha mgogoro wa madeni yameendelea kupata alama duni zaidi, ambapo tatizo hilo la mgogoro wa madeni limeonekana kama chachu ya vitendo vya rushwa. Ugiriki imepata alama 36, Italia 42, Ureno 63 na Uhispania 65.

Mkurugenzi Mkuu wa Transparency International, Cobus de Swardt, ameyataka mataifa yenye nguvu za kiuchumi duniani yanapaswa kuonesha mfano kwa kuhakikisha taasisi zake zinasimamia uwazi na kwamba viongozi wanawajibika katika hilo.

Mataifa ya Magharibi yanayoongoza kiviwanda, kama Uswis, Canada, Australia na Sweden yanashikilia tena ile nafasi yake ya kuwa safi katika kudhibiti tatizo la rushwa. Lakini China, kama taifa namba mbili kwa nguvu za kiuchumi duniani limepata alama 39.

Taifa kubwa kabisa lenye nguvu za kiuchumi duniani Marekani limepata alama 73 na Ujerumani, ambalo ni taifa lenye uchumi mkubwa kuliko yote barani Ulaya, ikiwa na alama 79. Urusi, pamoja na kuwa na utajiri mkubwa wa maliasili yake, inaonekana kufanya jitihada kidogo sana katika kukabiliana na tatizo la rushwa. Taifa hilo limeshika nafasi ya 133 katika nchi 176 katika kudhibiti rushwa kwa mujibu wa utafiti wa mwaka huu wa Transparency International.

Mwandishi: Sudi Mnette
Mhariri: Mohammed Khelef

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com