1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Australia yaipiku Argentina katika nusu fainali

26 Oktoba 2015

Australia imetinga hatua ya fainali ya michuano ya kombe la dunia la katika mchezo wa rugby baada ya kuichabanga Argentina pointi 29 dhidi ya 15.

https://p.dw.com/p/1Gu5B
IRB Rugby World Cup 2015 Halbfinale Australien Argentinien Rugby
Picha: Reuters/H. Browne

Mchezaji mahiri wa Australia Adam Ashley-Cooper, aliisaidia timu yake kupata alama 13 za kuongoza mchezo huu wa nusu fainali.

Australia itapamba na New Zealand katika mchezo wa fainali utakaofanyika Octoba 31 huku michezo ya mshindi wa tatu ikifanyika Octoba 30.

New Zealand ilifika fainali siku ya Jumamosi baada ya kuishinda timu ya Afrika Kusini kwa pointi 20 kwa 18.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP
Mharrii: Iddi Sessanga