1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rouhani iataka Japan kufanya upatanishi na Marekani

Sekione Kitojo
20 Desemba 2019

Rais wa Iran Hassan Rouhani ameishutumu Marekani kwa kujitoa katika makubaliano ya nyuklia na ameitaka Japan kusaidia   juhudi za kuendeleza makubaliano wakati viongozi hao wawili wa walipokutana mjini Tokyo.

https://p.dw.com/p/3V9oD
Japan | Iran | Shinzo Abe | Hassan Rohani
Picha: Getty Images/AFP/C. Triballeu

Rouhani , akiwa  ni  rais  wa  kwanza  wa  Iran  kufanya  ziara  nchini Japan  katika  kupindi cha miaka  miaka  19, alimwambia  waziri mkuu  Shinzo Abe  kuwa  makubaliano  ya  nyuklia  na  mataifa makubwa  duniani  bado  ni  muhimu.

Iran Teheran | Präsident Hassan Rouhani
Rais wa Iran Hassan Rouhani akiwa JapanPicha: picture-alliance/AA/Presidency of Iran

"Makubaliano  ya  nyuklia bado ni muhimu  sana  kwa  Iran. Kwa hiyo  nashutumu vikali  kujitoa kwa  Marekani ambako  ni  kwa upande  mmoja  na  bila  sababu. Nina  matumaini  Japan  na mataifa  mengine  yatafanya  juhudi  kuendeleza  makubaliano haya."

Abe  katika  matamshi  yake  ya  ufunguzi, ameitaka  Iran  kutekeleza kikamilifu  makubaliano  hayo na  kuchukua  juhumu  muhimu  katika kufanikisha  amani  na  uthabiti  katika  eneo  hilo. Abe  ameeleza wasi  wasi  wake  juu  ya  kuongezeka  kwa  hali  ya  wasi  wasi katika  mashariki  ya  kati  na  kuahidi  kuchukua  hatua  zaidi  kadri inavyowezekana  kulisaidia eneo  hilo kudumisha  uthabiti.

"Nina  matumaini  makubwa  kuwa  Iran  itatekeleza  kikamilifu makubaliano ya  nuklia, na  kuchukua  jukumu  muhimu  katika kuhimiza  amani  na  uthabiti  kwa  ajili  ya  kanda hiyo ya  mashariki ya  kati."

Japan | Iran | Shinzo Abe | Hassan Rohani
Rais wa Iran Hassan Rouhani akipokewa na mwenyeji wake waziri mkuu wa Japan Shinzo Abe mjini TokyoPicha: Reuters/C. Triballeu

Eneo  la  Mashariki  ya  kati  linaipatia  Japan kiasi  cha  asilimia  80 ya  mafuta. Japan , ambayo  ni  mshirika  wa  Marekani  ambae  ana mahusiano  ya  kiasili  na  Iran , pia  inataka  kuchukua  jukumu  la kuwa  mpatanishi  kati ya  Tehran na  Washington. Abe  amesema kuwa  jukumu  kama  hilo  linatarajiwa  na  jumuiya  ya  kimataifa.

Rouhani , ambaye  alikuwa  nchini  Malaysia  kuhudhuria  mkutano wa  mataifa ya  Kiislamu, aliwasili  mjini  Tokyo  leo  Ijumaa  mchana kwa  ziara  itakayomchukua  siku  nzima  na  kukutana  na  Abe  na kula  nae  chakula  cha  usiku, kwa  mujibu  wa  maafisa  wa  wizara ya  mambo  ya  kigeni  ya  Japan.

Hali  ya  wasi  wasi  imeongezeka  kati  ya  Iran  na  marekani  tangu pale  rais Donald Trump  kuchukua  uamuzi  mwaka  jana  kuiondoa nchi  yake  kutoka  katika  makubaliano  ya  kinyuklia  na  Iran mwaka ya  mwaka  2015.