1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ronald Koeman: Dhamira ya Messi Barcelona haimithiliki

5 Oktoba 2020

Barcelona walitetereka katika azma yao ya kupunguza mwanya baina yao na timu zilizo juu yao katika jedwali la ligi kuu nchini humo kwani hapo jana walizuiwa sare ya goli moja na Sevilla uwanjani kwao Camp Nou.

https://p.dw.com/p/3jSw7
Fußballspieler Lionel Messi 2018
Picha: picture-alliance/empics/N. Potts

Luuk de Jong ndiye aliyewafungia Sevilla katika dakika ya nane ila Philipe Coutinho alisawazisha baada ya kupokea pasi safi kutoka kwa Lionel Messi.

Kocha wake Ronald Koeman amesema Muargentina huyo amekuwa mfano kwa wachezaji wengine tangu alipoamua kusalia kuwa mchezaji wa Barca kwani kulikuwa na hofu kwamba hatojitolea kama awali kuichezea klabu hiyo baada ya uhamisho wake kuelekea Manchester City kuvunjika.

"Hakuna mjadala, kulingana na mimi amekuwa mchezaji bora duniani, nilikuwa na wazo hilo tangu kitambo na hata sasa ninapofanya kazi naye. Dhamira yake iko hapa kikamilifu na ni mfano kwa kila mmoja kwa jinsi nahodha anavyostahili kuwa," alisema Koeman.