1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rome.Treni zagongana na kusababisha vifo vya watu wawili na kadhaa kujeruhiwa.

17 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD1s

Treni mbili za chini ya ardhi zimegongana leo mjini Rome nchini Italy na kusababisha kuuwawa kwa watu wawili na kujeruhiwa kiasi cha 200 wengi wao wakiwa wameumia vibaya sana.

Ajali hiyo ilitokea wakati wa harakati za asubuhi katika moja ya kituo cha kusimama, katika kituo kikuu cha treni kwenye mji mkuu wa Italy, Rome.

Mashahidi wamesema kuwa treni moja ilivamia nyenziwe kwa nyuma baada ya kutofanikiwa kusimama wakati taa nyekundu ya kuiamuru isimame ilipokuwa ikiwaka.

Waokoaji bado wanaendelea kuwaokoa watu waliokwama katika mabaki ya treni hizo.

Kwa mujibu wa taarifa zilizokuwa hazijathibitishwa zimedai kuwa, umeme uliripuka wakati treni hizo zilipogongana.