ROME:Solana akutana na mjumbe mpya wa Iran | Habari za Ulimwengu | DW | 24.10.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

ROME:Solana akutana na mjumbe mpya wa Iran

Mjumbe mpya wa kimataifa wa Iran bwana Saeed Jalili amekutana na mkuu wa sera za nje wa Umoja wa Ulaya Javier Solana mjini Rome kujadili mgogoro wa nyuklia wa Iran.

Bwana Solana amesema mazungumzo yake na mjumbe huyo mpya yalikuwa na manufaa . Amefahamisha kuwa mazungumzo mengine yamepangwa kufanyika mwezi ujao.

Nchi muhimu duniani zimekubaliana kuchelewesha vikwazo dhidi ya Iran hadi mkutano huo utakapofanyika ili kuona iwapo Iran itakuwa tayari kushirikiana na shirika la kimataifa la kudhibiti matumizi ya nishati ya nyuklia IAEA.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com