1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ROME:Italia yakiri askari wake kutoweka nchini Afghanistan

24 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBN9

Italia imethibitisha kuwa wanajeshi wake wawili huko nchini Afghanistan hawajulikani waliko.

Mapema polisi wa Afghanistan walisema kuwa wako katika msako wa kuwatafuta wanajeshi hao akiwemo dereva na mkalimani wao baada ya kutoweka katika wilaya ya Shindad kwenye jimbo la magharibi la Herat.

Wanajeshi hao walikuwa katika kikosi cha ujenzi cha jeshi la kujihami la nchi za Magharibi NATO nchini Afghanistan.

Mjini New York katika Umoja wa Mataifa, wanadiplomasia kutoka nchi 18 wanajadiliana juu ya njia za kusaidia juhudi za kimataifa za kurejesha utulivu na kuijenga upya Afghanistan.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amemtaka Rais wa Afghanistan Hamid Karzai kuweka utawala bora na kupambana na rushwa pamoja na biashara ya madawa ya kulevya.