ROME:Baba Mtakatifu Benedikt wa 16 leo atimia umri wa miaka 80 | Habari za Ulimwengu | DW | 16.04.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

ROME:Baba Mtakatifu Benedikt wa 16 leo atimia umri wa miaka 80

Baba Mtakatifu Benedikt wa 16 leo anatimiza umri wa miaka 80 baada ya kuadhimisha siku hiyo jana pamoja na maalfu ya waumini wa kanisa katoliki kwenye uwanja wa mtakatifu Peter mjini Rome.

Wakati huo huo mwakilishi wa baba mtakatifu nchini Israel amehudhuria maadhimisho yanayofanyika kila mwaka nchini humo kukumbuka maangamizi ya wayahudi.

Hapo awali mwakilishi huyo askofu Antonio Franco alitishia kususia maadhimisho hayo kutokana na kukasirishwa na kichwa cha habari kilichondikwa kwenye nyumba ya makumbusho kilichosema kuwa baba mtakatifu wa wakati huo, Pius wa 12 alinyamaa kimya hata baada ya habari juu ya kungamizwa kwa wayahudi kufika Vatikan.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com