ROMA:Hali ya ukame yaifanya Italia kutangaza hali ya dharura | Habari za Ulimwengu | DW | 04.05.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

ROMA:Hali ya ukame yaifanya Italia kutangaza hali ya dharura

Italia imetangaza hali ya dharura katika maeneo ya kaskazini na kati ya nchi hiyo kutokana na hofu ya ukame kufuatia hali mbaya ya hewa.

Waziri wa Mazingira wa Italia Alfonso Pecoraio Scanio, amesema kuwa hali hiyo imetangazwa kama hatua za tahadhari.

Hatua hiyo imekuja siku moja baada ya nchi jirani na Italia, Ufaransa, kutangaza mgawo wa maji katika maeneo kadhaa ya nchi hiyo kwa hofu pia ya ukame.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com