1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Robo fainali ya UEFA Champions League kuanza kutimua vumbi

7 Aprili 2026

Mabingwa wa Ujerumani Bayern Munich watakuwa ugenini kumenyana na mabingwa wa mara nyingi wa kombe hilo, Real Madrid. Arsenal watawakaribisha Sporting Lisbon ya Ureno katika uwanja wao wa nyumbani wa Emirates.

https://p.dw.com/p/5BkYp
Kane I Bayern
Nyota wa Bayern Munich Harry Kane akishangilia goliPicha: Thilo Schmuelgen/REUTERS

Michuano ya Ligi ya mabingwa barani Ulaya maarufu UEFA Champions League katika hatua ya robo fainali inaanza kutimua vumbi hii leo katika viwanja mbalimbali. Mabingwa wa Ujerumani Bayern Munich watakuwa ugenini kumenyana na mabingwa wa mara nyingi wa kombe hilo, Real Madrid.

Vinara wa ligi kuu ya Premia nchini England, Arsenal watawakaribisha Sporting Lisbon ya Ureno katika uwanja wao wa nyumbani wa Emirates.

Mechi nyingine za hatua hiyo ya robo fainali ya UEFA Champions League zinatarajiwa kuendelea hapo kesho ambapo mabingwa watetezi wa kombe hilo Paris Saint German watawakaribisha Liverpool huku Barcelona wakiwa nyumbani kumenyana na Atletico Madrid zote za Uhispania.

Mechi za marudiano za hatua hiyo ya robo fainali zitachezwa wiki ijayo.