1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Robinho-stadi wa Brazil mbaroni ?

28 Januari 2009

Eti kweli amembaka msichana ?

https://p.dw.com/p/Gi2O
Brazil's RobinhoPicha: AP

Stadi wa Brazil Robinho anaeichezea Manchester City,alikamatwa na baadae kuachwa huru huko Uingereza, kwa tuhuma za eti alimbaka msichana wa miaka 18 katika klabu cha starehe mjini Leeds, wiki 2 zilizopita.

Robinho binafsi, alikanusha jana mashtaka hayo.

Watoto 2 wakike wa Rais Barack Obama watakabidhiwa jazi 2 zenye majina yao na nambari 20 na 44-siku ya kutawazwa Rais Obama Januari 20 na ya kuwa rais wa 44 wa Marekani.

Kesi ya uhalifu juu ya kashfa iliopita katika Ligi ya itali 2006 ya kupanga matokeo ilisikilizwa jana na mara kuahirishwa na jiji la Madrid limepongezwa kwa maandalio yake hadi sasa m iongoni mwa miji inayoania kuandaa olimpik 2016.

Robinho,mchezaji ghali kabisa katika Premier League-ligi ya Uingereza alikamatwa kwa tuhuma eti za kumbaka msichana wa miaka 18 huko Leeds wiki 2 zilizopita.

"tunaweza kuthibitisha kwamba Ribinho alikutana na polisi leo kama ilivyoafikiwa kabla na sehemu ya uchunguzi wa kitendo cha uhalifu." msemaji wa Robinho, Chris Nathaniel aliarifu.

Lakini alikanusha vikali tuhuma zozote za kufanya makosa au kitendo cha kihalifu na yutayari kushirikiana na polisi endapo atahitajika zaidi.Polisi ya Yorkshire ya magharibi imehakikisha kukamatwa lakini ikifuata desturi yake,haikutaja jina la aliekamatwa.

Robinho ambae jina lake hasa ni Robinson de Seouza,alikuwa mchezaji wa dimba alienunuliwa kwa kitita kikubwa kabisa nchini Uingereza kuliko yeyote yule : pauni 32 milioni sawa na dala milioni 45.15 na Manchester City.

Alikombolewa kwa kitita hicho kutoka klabu yake ya zamani ya Real madrid,nchini Spian.

Wiki iliopita,Robinho aliondoka katika kambi ya mazowezi ya Manchester City huko Tenerrife,Spain bila ya ruhusa na kurejea Brazil.Aliporejea kocha wa Manchester City Mark hughes kwanza alidai Robinho atachukuliwa hatua ya nidhamu.

Katika Serie A,Ligi ya Itali, mashtaka ya uhalifu wa ile kashfa ya kupanga matokeo ya mechi iliotikisa dimba la Itali mwaka wa Kombe la dunia 2006, ilianza jana na hapo hapo kuahirishwa hadi mwezi Mach mwaka huui.Luciano Moggi,meneja mkuu wa zamani wa klabu ya Juventus na washtakiwa wengine 23 , wanakabili mashtaka yanayojumuisha udanganyifu.

Kocha wa Arsenal amesema jana kwamba, klabu yake haikuwafiki kitita kinachodaiwa ili kumuajiri stadi wa urusi wa dimba Andrei Arshavin. Klabu ya Arshavin, Zenit St.Petersberg ya Urusi,iliarifu juzi kwamba ni masharti tu ya kumuajiri stadi hiyo ndio yaliosalia kutatuliwa.Wenger,kocha wa Arsenal anakanusha kuwapo maafikiano yoyote juu ya malipo.

Taarifa kutoka Madrid,Spian zinasema kuwa,wasichana wawili wa Rais Barack Obama, wanaripotiwa karibuni hivi watakabidhiwa zawadi ya jazi 2 kutoka klabu ya Sevilla ya Spian.Sevilla imejiunga na mkumbo wa Obama na umetoa jazi zenye majina ya watoto wa rais huyo wa Marekani zikiwa na namba 20 na 44: Namba 20 ni siku aliotawazwa baba yao Barack Hussein Obama rais wa Marekani na 44 ni rais wa 44 wa Marekani.

Kwa muujibu wa desturi za kimataifa ,Sevilla imewapeleka jazi hizo kupitia Balozi wa Spian, nchini Marekani ili azikabidhi Ikulu. Watoto hao wakike wa rais Obama wamesema ni mashabiki wa dimba.

Mwishoe, michezo ya olimpik ya mwaka 2016:

Madrid, jiji kuu la Spain liko usoni kwa maandalio mazuri miongoni mwa miji inayogombea kuandaa.Madrid imepongezwa na mashirikisho yote 26.Madrid inachuana na miji ya tokyo,Chicago na Rio de Jeneiro kupata haki ya kuandaa Olimpik 2016.