Robben arejea katika kikosi cha Bayern | Michezo | DW | 21.03.2015
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Michezo

Robben arejea katika kikosi cha Bayern

Bayern Munich itateremsha tena uwanjani na mchezaji wake wa pembeni katika safu ya mashambulizi na mfungaji wake mkubwa Arjen Robben katika pambano lake la Bundesliga dhidi ya Borussia Monchengladbach

Mholanzi huyo aliwekwa kando wakati wa pambano la wiki iliopita ambapo Bayern ilitandika bila vibaya werder Bremen mabao 4-0. Robben aliumia mgongo wakati wa mchezo wa marudiano na Shakhtar Donetsk ya Ukraine la kombe la vilabu bingwa la Ulaya Champions League . Donetsk ilitandikwa bila huruma mabao 7-0 na kuyaaga mashindano hayo.

Robben mwenye umri wa miaka 31 ameshafunga mabao 17 katika ligi kuu msimu huu na anamatumaini kuwemo katika kikosi kitakachochuana na Borussia Dortmund Aprili 4 na siku nne baadae katika mchezo wa robo fainali ya Kombe la Ujerumani dhidi ya Bayer Leverkusen, kabla ya pambano la kwanza la robo fainali ya kombe la Ulaya champions League kati ya Aprili 14 na 15.

Mechi nyengine kesho, Wolfsburg inayoshika nafasi ya pili katika msimamo wa igi hiyo watakuwa wageni wa Mainz. timu zinazokabiliwa na hatari ya kushuka daraja ni Paderborn, Freiburg na Stuttgart inayokamata mkia.

Mwandishi: Mohammed Abdul-Rahman, rtre, afp
Mhariri: Saumu Yusuf

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com