RIYADH : Sudan na Chad zafikia usuluhishi | Habari za Ulimwengu | DW | 04.05.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

RIYADH : Sudan na Chad zafikia usuluhishi

Sudan na Chad zimetia saini makubaliano ya usuluhishi nchini Saudi Arabia hapo jana zikiahidi ushirikiano na Umoja wa Mataifa katika kuleta utulivu kwenye jimbo la Dafur nchini Sudan na katika maeneo ya jirani nchini Chad.

Afisa wa Saudia akisoma taarifa ya makubaliano hayo amesema kwamba pande hizo mbili zimeahidi kushirikiana na Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa kukomesha mzozo huko Dafur na mashariki mwa Chad ili kuleta utulivu na amani kwa wote.

Amesema makubaliano hayo yaliosainiwa na Rais Omar Hassan al Bashir wa Sudan na mwenzake wa Chad Idriss Deby yanaelezea kuheshimu haki ya kujitawala kila mmoja kwa mwenzake, kutoingilia kati masuala ya ndani ya nchi au kuwapa hifadhi vikosi vya upinzani na kuvitimua vikosi hivyo mara moja.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com