1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rishi Sunak na Emmanuel Macron kujadili uhamiaji na Ukraine

Tatu Karema
9 Machi 2023

Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak anatarajiwa kumtembelea rais wa Ufaransa Emmanuel Macon, kuimarisha ushirikiano wao juu ya uhamiaji, Ukraine na kuanzisha mwanzo mpya hasa baada ya miaka ya mizozo ya Brexit.

https://p.dw.com/p/4OStA
Cop27 -  Rishi Sunak und Emmanuel Macron
Picha: Steve Reigate/Daily Express/empics/picture alliance

Katika mazungumzo mjini Paris, Sunak ambaye alichaguliwa waziri mkuu mwezi Oktoba, atategemea kutumia fursa hiyo kukomesha miaka kadhaa ya mzozo kuhusu masuala kuanzia uhamiaji hadi uvuvi.

Uhusiano kati ya mataifa hayo uliogeuka kuwa wa uhasama tangu Uingereza ilipopiga kura kuondoka Umoja wa Ulaya mwaka 2016, umeimarishwa na uungaji mkono wa mataifa hayo mawili kwa Ukraine tangu uvamizi wa Urusi, na mkutano huo unatazamwa kama fursa ya kuuimarisha zaidi.