RIPOTI YA MAREKANI JUU YA IRAQ | Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili | DW | 13.07.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Timu Yetu

RIPOTI YA MAREKANI JUU YA IRAQ

Baraza la waakilishi la Marekani limepioga kura kutaka majeshi ya Marekani nchini Irak yarudishwe nyumbani hadi April mosi, mwakani. Rais Bush ametishia kulitia munda azimio hilo.

Likiwa halikujali kitisho cha rais Bush kulizima kwa kura yake ya veto,Baraza la waakilishi la Marekani limepitisha jana mswada unaodai majeshi ya Marekani yaondoke Irak mnamo muda wa siku 120 na yakamilishe mpango wa kuhama hadi April mosi,mwakani.

Baraza hilo liliiidhinisha mswada huo kwa kura 223 dhidi ya 201.Wajumbe 4 wa chama cha repuiblican cha rais Bush wamelipigia kura azimio hilo.Wabunge 10 wa chama cha upinzani cha Democrat hawakulipigia kura.

Akijitetea, rais George Bush alidai jana kwamba Marekani yaweza bado kushinda vita hivi vya Iraq vilivyodumu miaka 4 sasa na akaonya kuwaondosha Iraq wanajeshi 160.000 wa marekani maana yake itakuwa kusalim-amri mustakbala wa Irak na kuweka mikononi mwa Al Qaeda.

Akaongeza kwamba yungali ana imani na waziri mkuu Al maliki na akaapa hatatoa hukumu ya mwisho ya jinsi viota vinavyokwenda hadi kwanza amepta ripoti ya kamanda wa Marekani nchini Iraq,jamadari David Petraeus hapo Septemba.

“Naamini tunaweza kufaulu nchini Iraq; na najua lazima tufaulu.Kwani, tunapigana kuishinda Al Qaeda na wengine wenye siasa kali na tunasaidia kusimama serikali ya Iraq itakayoweza kuwalinda watu wake,kuwapatia huduma muhimu na kuwa mshirika wetu katika vita dhidi ya siasa na

Vita vya Iraq vimeua askari si chini ya 3,612 wa Marekani.

Ripoti iliotoka hivi punde imebainisha kwamba juhudi za Iraq kuvijenga vikosi vyake ili kumudu kusimamia usalama bila ya msaada wa Marekani –shabaha muhimu ya Washington-haziridhishi.Isitoshe, ripoti imesema masharti ya kwanza ya kuwa na mpango wa kuwapokonya silaha wanamgambo hayapo kabisa.

Rais Bush lakini akitapatapa kudhibiti mamlaka yake yanayomponyoka hatua kwa hatua mwishoni mwa awamu yake ya pili ya urais,alitetea maamuzi yake

Juu ya Irak kuwa barabara.Akasema,

“Wale wanoamini kuwa vita nchini Iraq vimeshindwa yamkini wakataja kule kutotekelezwa kwa baadhi ya shabaha za kisiasa zilizolengwakufikiwa.

Na wale miongoni mwetu wanoamini kuwa vita nchini Iraq vinaweza kuleta ushindi na lazima vilete ushindi huo,wanayona mafanikio yaliopatiukana upande wa shabaha kadhaa za kuleta usalama zilizolengwa kuwa ni chanzo cha matumaini.”

Rais Bush ametangaza juhudi mpya ya diplomasia juu ya vita vya Iraq kwa kumtuma waziri wake wa mambo ya nje Dr.Condoleeza Rice na waziri wa ulinzi Robert Gates Mashariki ya kati mwezi ujao kushauriana na washirika juu ya vita hivi.

Bush akaungama:

Kwanza, naelewa kwanini wananchi wa marekani wamechoshwa na vita hivi.Kuna machofu ya kweli ya vita nchini Marekani.Naelewa hivi ni vita vichafu……”

Mshirika wa chanda na pete wa Marekani katika vita vya Irak imekuwa Uingereza.Jana, waziri wake wa maendeleo ya kimataifa,Dpuglas Alexander, ametoa ishara ya badiliko katika siasa za nje za uingereza kuelekea mshirika wake Marekani.Alisema nguvu za dola zinategemea mno kuwa zaidi na marafiki kuliko nguvu za kijeshi.

Akasema na ninamnukulu,

“Katika karne ya 20,nguvu za dola mara nyingi zikipimwa kwa uwezo wake wa kuangamiza.Katika karne ya 21,nguvu zapaswa kupimwa juu ya kile tunachoweza kujenga pamoja.”

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com