1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ripoti: Usafiri wa anga ulikuwa shwari 2017

2 Januari 2018

Kwa mujibu wa wataalamu wa usafiri wa anga, mwaka 2017, ulikuwa mwaka salama zaidi katika rekodi  kwa abiria wanaotumia usafiri wa anga.  Hakukuwa na ajali mbaya za ndege za abiria kwa mwaka 2017.

https://p.dw.com/p/2qEIc
Jacdec Sicherheitsranking Luftfahrtgesellschaft Hong Kong Airlines
Picha: picture-alliance/dpa/C. Kang

Mtandao wa Usalama wa Anga(ASN) umefanya utafiti na kubaini kuwa, mwaka 2017, ulikuwa mwaka salama kwa usafiri wa anga. Usafiri wa anga haukuwa na ajali yoyote iliyosababisha vifo katika ndege za abiria za biashara kwa mwaka jana. Hayo ni kwa mujibu wa ripoti mbili zinazojitegemea, zilizotolewa mwanzoni mwa huu  2018.

Kampuni ya ushauri wa usafiri wa anga ya Kijerumani, To70 na Mtandao wa Usalama wa Usafiri wa anga(ASN) walithibitisha kuwa hakukuwa na ajali mbaya ya ndege za abiria kwa mwaka 2017. ``Mwaka  uliopita 2017, ulikuwa mwaka salama kwa usafiri wa anga``  Adrian Young wa To70  aliliambia Shirika la Habari la Reuters.

Passagierflugzeug Bombardier DHC-8-400 der Air Berlin
Picha: picture-alliance/W. Mendorf

Kwa upande wake Rais wa  mtandao ASN; Harro Ranter, alisema kwa wastani,  tangu mwaka1997, idadi ya ajali za usafiri wa anga,  imepungua kwa kasi. 

Kwa kiasi kikubwa, alishukuru juhudi za kusimamia usalama zinazofanywa na Taasisi za kimataifa  za mashirika ya usafiri wa anga, ikiwamo ICAO; IATA; na Flight Safety Foundation na kiwanda cha usafiri wa anga.

Vifo vinavyotokana na ajali za ndege, duniani, vimepungua kwa kasi katika miongo miwili iliyopita. ASN imesema mwaka 2005, haukuwa na vifo zaidi ya 1000 vinavyotokana na ndege za abiria kwa mwaka duniani kote. Taasisi ya To70  inakadiria kuwa  kiwango cha  ajali mbaya kwa ndege kubwa za abiria, kwa sasa ni 0.06 kwa ndege milioni moja, au ajali moja kwa kila ndege 16 milioni.

 Tahadhari yatolewa kwa ajali za usafiri wa anga

Hata hivyo bado hatari ipo. Taasisi hizo mbili hazikukubaliana na  hesabu  ya ajali mbaya kwa mwaka 2017. Wakati  taasisi ya  To70 ikiripoti ajali mbili mbaya za ndege, zilizohusisha ndege ndogo, ASN, ilidai kulikuwa na ajali 10 mbaya  za ndege, zilizosababisha vifo vya abiria 44 na 35 kujeruhiwa.(on the ground)

Mtandao wa ASN uliongeza kuwa hata hivyo, ajali za ndege za mizigo, zilizohuisha watu zilijumuishwa katika idadi hiyo, wakati matukio ya usafiri wa anga wa kijeshi, hayakujumuishwa.

 Ilisisitizwa kuwa, hata ukizingatia matukio hayo, bado mwaka 2017, unabaki kuwa mwaka wenye idadi ndogo ya vifo vitokanavyo na  ajali katika historia ya usafiri wa anga kwa sasa.

 Wakati huo huo, To70 ilisisitiza kuwa, hata ajali ambazo hazikusababisha vifo bado ziliendelea kuwa tishio. Ni kutokana na matukio ya kufeli kwa injini  ajali nyingine zinazohusiana na injini, ambayo sekta ya usafiri wa anga inapaswa kujiimarisha. 

Kadhalika imesisitiza kuwa dosari nyingine za kiusalama zimeongezeka katika miaka ya karibuni, ikiwamo ongezeko la moto unaosababishwa na betri za lithium-ion, unaopatikana katika vifaa vya umeme kama simu za mkononi  zinazobebwa katika ndege.

Star Alliance Gründungsmitglieder Flugzeuge
Picha: picture-alliance/dpa/O. Berg

Kadhalika mwaka 2017,    ndege ya Shirika la Ndege la Canada, Air Canada, iliponea chupuchupu  kupata ajali katika tukio lililobatizwa jina la ´janga kubwa la usafiri wa anga´, baada ya ndege hiyo, almanusura kutua  juu ya ndege nyingine nne, zilizokuwa katika barabara ya ndege kwenye Uwanja wa ndege wa San Francisco nchini Marekani .

Mwandishi: Florence Majani (http://www.dw.com/en/2017-the-safest-year-on-record-for-air-passengers/a-41993923)

Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman.