Ripoti: Roberto Di Matteo atimuliwa na Schalke | Michezo | DW | 25.05.2015
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Ripoti: Roberto Di Matteo atimuliwa na Schalke

Ndoa kati ya Schalke na Roberto Di Matteo imekuwa ya muda mfupi. Magazeti kadhaa ya Ujerumani yameripoti kuwa Schalke imemfuta kazi Mkufunzi huyo Muitaliano

Habari kuwa Roberto Di Matteo ameachishwa kazi na Schalke zilitolewa jana jioni na jarida la michezo la Ujerumani “SportBild” na kuthibitishwa na gazeti jingine linaloheshimika sana la “Frankfurter Allgemeine Zeitung” pamoja na jarida la kandanda la “Kicker”.

Klabu hiyo haijathibitisha wala kukanusha habari hizo, na pia hakuna habari zozote kuhusu atakayechukua nafasi yake. Di Matteo alichukua usukani kutoka kwa Jens Keller mnamo Oktoba saba 2014. Walishindwa kufuzu katika ligi ya mabingwa na hata mashabiki wakaanza kunung'unika dhidi ya mfumo wake wa kandanda lisilovutia.

Mwandishi: Bruce Amani
Mhariri: Yusuf Saumu