1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Riga: Wanachama wa NATO watakiwa kuchangia wanajeshi zaidi

28 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCoY

Wakati viongozi wa Jumuiya ya kujihami ya magharibi NATO wakikutana katika mji mkuu wa Latvia-Riga, katibu mkuu wa jumuiya hiyo Jaap de Hoop Scheffer ameyataka mataifa mengi zaidi wanachama kuchangia maelfu ya wanajeshi kusini mwa Afghanistan.Kwa wakati huu ni wanajeshi wa Uingereza, Canada na Uholanzi wanaopambana na waasi wa Taliban. Ujerumani na Uhispania imeweka wanajeshi wao katika mikoa mengine kwenye hali ya utulivu. Bw Scheffer alisema NATO haiwezi kuwa na kile kinachoitwa jeshi la ujenzi mpya, ikiwa itashindwa kukabiliana na mapambano.