1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

RIGA: Ulaya kushinikizwa kusaidia zaidi Afghanistan

27 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCou

Kuibuka upya kwa kundi la Taliban nchini Afghanistan ni suala muhimu katika mkutano wa viongozi wa Umoja wa Kujihami wa Mataifa ya Magharibi NATO unaofunguliwa hapo kesho huko Riga nchini Latvia .

Machafuko ya umwagaji damu nchini Afghanistan yamefikia hali mbaya kabisa kuwahi kushuhudiwa tokea vikosi vinavyoongozwa na Marekani na Uingereza kuupinduwa utawala wa Taliban hapo mwaka 2001.

Rais George W Bush wa Marekani ambaye ameondoka mjini Washington leo asubuhi na kutuwa kwanza huko Estonia atazihimiza nchi za Ulaya kuongeza vikosi vyao nchini Afghanistan pamoja na kuondowa vikwazo walivyoviwekea vikosi hivyo nchini humo.

Akizungumzia suala hilo la Afghanistan Katibu Mkuu wa NATO Jaap de Hoop Sheffer amesema NATO inahitaji washirika wa dunia.

Marekani,Uingereza na Canada zinalalamika kwamba zimekuwa zikibeba mzigo mkubwa wa NATO katika sehemu za vurugu kama vile kusini mwa nchi hiyo.