Reus ang′aka kuhusu ukomavu wa BVB | Michezo | DW | 23.09.2019
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Reus ang'aka kuhusu ukomavu wa BVB

Kinyang'anyiro cha ligi kuu ya kandanda ya Ujerumani Bundesliga kimeendelea kushika kasi, wakati RB Leipzig inayonuia kuonyesha uwezo wake kwenye msimu huu ikiendelea kung'ang'ania kileleni mwa ligi.

Bayern Munich mabingwa watetezi walikaa kileleni kwa muda mfupi baada ya kuichabanga FC Köln mabao 4-0. RB Leipzig waliocheza pungufu walifanikiwa kuwashusha hadi nafasi ya pili kufuatia ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Bremen. Leipzig inaongoza kwa pointi 13, Munich pointi 11 na Freiburg ikishika nafasi ya tatu ikiwa na pointi 10.

Borussia DortmundBayern Munich yashikwa shati, BVB yapanda imeporomoka hadi nafasi ya tatu kufuatia sare ya mabao 2 kwa 2 walipokaribishwa na Eintracht Frankfurt. Nahodha Marco Reus, amepinga vikali ukosoaji dhidi ya kikosi hicho kwamba hakina ari ya kutafuta ushindi hata baada ya sare ya bila kufungana na Barcelona katika michuano ya klabu bingwa barani Ulaya, Champions League. Reus alinukuliwa aking'aka "Inanikasirisha, na maoni hayo ya hovyo kuhusu ukomavu wa kikosi chetu" aliwajibu waandishi wa habari waliomuuliza kuhusu iwapo kikosi chake kina tatizo la ukomavu. Reus aliwaonya waandishi hao kutoendelea na maswali hayo aliyoyaita ya kipuuzi kuhusu kikosi cha Dortmund.

Michezo mingine ya Bundesliga iliwakutanisha Schalke 04 iliyoshinda 2-1 dhidi ya Mainz, Leverkusen ilipata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Union Berlin, huku Borussia Moncheglabach ikiponyoka na pointi tatu ilipokutana na Fortuna Dusseldorf. Hofu ingali dhahiri kwa timu iliyopanda daraja ya Padermon, ambayo inaburuta mkia, na wasiwasi ukiwa iwapoa itasalia kwenye ligi kuu msimu ujao ama la.