Real na Atletico zatoshana nguvu mkondo wa kwanza | Michezo | DW | 20.08.2014
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Real na Atletico zatoshana nguvu mkondo wa kwanza

Goli la kusawazisha lililofungwa na Raul Garcia ikiwa imesalia dakika mbili mechi kukamilika lilimnyima James Rodriguez fursa ya kuwa na mwanzo mzuri katika uwanja wa nyumbani wa Santiago Bernabeu.

Hii ni baada ya Real Madrid kulazimika kukubali sare ya goli moja kwa moja na Atletico Madrid katika mchuano wa mkondo wa kwanza wa Super Cup ya Uhispania.

La kushangaza ni kuwa Rodriguez alianza kama mchezaji wa akiba, lakini akaingia kama nguvu mpya kuchukua nafasi ya Cristiano Ronaldo baada ya kipindi cha kwanza wakati mshindi huyo wa tuzo ya mchezaji bora wa mwaka alipolazimika kuondolewa uwanjani kutokana na maumivu ya jeraha lake linalomtatiza la goti.

Rodriguez alifunga goli la ikiwa imesalia dakika 10 mecho kuisha. Lakni Atletico walipata bao muhimu la ugenini ili kuufanya mchuano wa marudiano wa Ijumaa hii kuwa wa kuvutia hata zaidi nyumbani kwa Atletico, Vicente Calderon. Hii ni baada ya Raul Garcia kufunga goli kutokana na mkwaju wa kona. Vijana wa Carlo ANCELOTTI waliumiliki mchezo kwa kipindi kirefu lakini hawakuonekana kufayna mashambulizi ya kutatiza katika lango la Atletico.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP
Mhariri: Yusuf Saumu