Real Madrid, Man United kukabiliwa na mtihani Champions League | Michezo | DW | 11.02.2019
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Real Madrid, Man United kukabiliwa na mtihani Champions League

Kinyang'anyiro kitamu zaidi na cheye hadhi kubwa katika kandanda la vilabu kinarejea tena huku kukiwa na mechi kadhaa za kumezea mate za hatua ya 16 bora.

Mabingwa watetezi Real Madrid ambao wanaonekana kuanza kupata matokeo mazuri chini ya kocha Santiago Solari, watakuwa Uholanzi kuvaana na Ajax Amsterdam siku ya Jumatano baada ya kuwapiga mahasimu wao wa mjini Atletico Madrid 3 – 1 na kuruka hadi nafasi ya pili kwenye jedwali la La Liga. Kiungo Isco atakuwa nje ya mchezo kutokana na matatizo ya shingo na mgongo. Kocha Solari hata hivyo atakuwa na uamuzi mgumu wa kufanya katika kuchagua kati ya Gareth Bale na chipukizi Vinicius Junior.

Borussia Dortmund watawatembelea Tottenham Hotspur uwanjani Wembley kesho Jumanne katika mpambano kati ya ligi ya Premier ya England na Bundesliga ya Ujeurmani. Spurs watakuwa bila ya washambuliaji Harry Kane na Dele Alli.

Roma watawaalika Porto kesho katika mechi nyingine ya mtoano wiki hii lakini macho yote yatamulikwa uwanjani Old Trafford wakati mfululizo wa ushindi wa United katika mechi 10 kati ya 11 tangu kocha Ole Gunnar Solskjaer alipochukua mikoba ya Mourinho utafanyishwa mtihani mkali na mabingwa wa Ufaransa PSG. PSG watakosa huduma za Neymar pamoja na mshambuliaji mwenzake Edinson Cavani ambao wako mkekani.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA
Mhariri: Josephat Charo